SADC yaitaka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuunda serikali ya muungano ili kuzuia machafuko.

In Kimataifa

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi Kusini mwa Afrika, SADC, imetoa wito kwa viongozi wote wa kisiasa katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuzingatia majadiliano na kuunda serikali ya muungano. Mwenyekiti wa SADC Edgar Lungu ametoa wito huo kutokana na hofu ya kuzuka machafuko katika Jamhuri hiyo. Lungu amesema serikali za muungano zimefanikiwa katika nchi kadhaa za Afrika kama Afrika Kusini, Zimbabwe na Kenya. Amesema pia tayari amezungumza na Feliy Tshisekedi aliyetajwa mshindi wa uchaguzi huo pamoja na washikadau wengine wakiwemo wale walioko katika maeneo ya Maziwa Makuu. Kulingana na Lungu jumuiya ya SADC imezingatia mashaka yaliyotolewa na Kanisa Katoliki nchini Congo ambalo lilikuwa na waangalizi zaidi ya 40,000 katika uchaguzi huo. Mapema Ijumaa tume ya uchaguzi ilimtangaza Tshisekedi kama aliyeshinda kwa asilimia 38.57 ya kura. Mpinzani wake Martin Fayulu amewasilisha rufaa katika mahakama ya katiba mjini Kinshasa akisema matokeo ya kura hiyo yalikuwa yamechakachuliwa.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

TCRA yatoa leseni 224 za watoa huduma za maudhui mtandaoni…93 ni za Blogs, 97 ni za Online Tv.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba amesema leseni 224 zimetolewa kwa watoa huduma

Read More...

Muungano wa Afrika umeiomba DR Congo uahirishe kutangaza matokeo kamili ya uchaguzi mkuu

Muungano wa Afrika (AU) umeitaka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo iahirishe kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu. Muungano huo unaonuia

Read More...

Bunge kupiga kura tena 29 mwezi januari.

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ataitisha kura nyingine Januari 29 kuhusu makubaliano ya Uingereza kujitoa kutoka Umoja wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu