SALAH ATAKA MKWANJA MREFU

In Kimataifa, Michezo

Mshambuliaji wa kikosi cha Liverpool Mohamed Salah
amewaambia mabosi zake kuwa anataka kupewa mshahara
mnono ili afanye kazi kwa raha akiwa ndani ya kikosi hicho.

Nyota huyo raia wa Misri uwezo wake ni wa hali ya juu na ni
miongoni mwa washambuliaji wanaopendwa na mashabiki wa
Liverpool pamoja na benchi la ufundi na anatajwa kuwa kwenye
rada za timu mbalimbali Ulaya zinazowinda saini yake.


Salah anataka kuwa mchezaji ambaye analipwa mkwanja mrefu
zaidi kwenye timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Jurgen
Klopp ambaye hivi karibuni alieleza kuwa amefanya
mazungumzo na nyota huyo kuhusu kuongeza mkataba mpya.
Kwa sasa kinara anayelipwa mkwanja mrefu ndani ya Liverpool
ambayo ni timu kubwa Ulaya ni beki wao wa kati kitasa Virgil
van Dijk ambaye analipwa pauni 220,000 kwa wiki na Salah
anataka awe anakunja pauni 500,000 kwa wiki.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tetesi za Soka Ulaya leo Alhamisi Septemba 23, 2021

Mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette, 30, hana hamu ya kusaini kandarasi mpya klabuni hapo. Mkataba wake wa

Read More...

Wanaharakati wa haki za binadamu wahoji hukumu dhidi ya Rusesabagina

 Makundi ya kutetea haki za binadamu barani Afrika yamelalamikia uamuzi wa mahakama kuu ya Rwanda ya kumfunga jela kwa miaka 25, Paul Rusesabagina ambaye alisifika sana kwenye filamu ya Hollywood ya Hotel Rwanda.  Mahakama hiyo Jumatatu ilisema kwamba imepata Rusesabagina pamoja na washukiwa wengine 20 na hatia ya

Read More...

LISSU NA WENZAKE WAFUTIWA KESI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeifutia kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleao

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu