Sekta ya kilimo kuleta mageuzi makubwa.

In Kitaifa

WIZARA ya Kilimo imelieleza Bunge kuwa, mwelekeo wa sekta ya kilimo itakaousimamia kuanzia sasa hadi mwaka 2025 ni kuleta mageuzi ya kilimo kutoka mtazamo wa kilimo cha kujikimu kwenda kwenye mfumo wa kilimo cha kibiashara.

Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Charles Tizeba amesema, lengo la mageuzi hayo ni kuhakikisha shughuli za kilimo zinakuwa na manufaa kwa nchi na wakulima kuendana na dhamira ya kufikia uchumi wa kati na wa viwanda.

“Napenda kutoa shukurani za pekee kwa wakulima wa nchi hii kwa kazi kubwa wanayofanya katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara” amesema.

Waziri Tizeba amesema, kilimo ni muhimu kwa maisha na ustawi wa uchumi kwa watu wengi nchini na ni nyenzo muhimu katika mapambano dhidi ya umasikini, kupanua fursa za ajira, kushirikisha wananchi wengi katika mnyororo wa thamani na biashara kimataifa na ni msingi wa mageuzi kuelekea uchumi wa viwanda na kipato cha kati.

Amesema, mchango wa kilimo katika ukuaji uchumi na ustawi wa jamii hauendani na fursa kubwa iliyopo na kwamba kwa kiasi kikubwa hali hiyo inachangiwa na mambo yaliyo ndani ya uwezo wa Watanzania yakiwemo mawazo mgando kuhusu uendeshaji sekta hiyo.

“Namshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kuanza utekelezaji wa hatua hii ya mageuzi kwa ari na mifano ya dhati. Mheshimiwa Rais ametoa maelekezo ya kuondoa kero na vikwazo visivyostahili walivyowekewa wakulima kwa miaka mingi…”amesema Dk. Tizeba.

Amesema, sekta ya kilimo inaajiri zaidi ya ya asilimia 65 ya nguvukazi nchini na pia asilimia 80 ya Watanzania masikini wanaishi kwa kutegemea kipato kinachotokana na kilimo.

“Kwa mantiki hiyo, mageuzi tunayotaka kuyafanya ni ya kuondoa asilimia 80 ya Watanzania walio katika lindi la umasikini, au kiasi cha watu milioni 10 ifikapo mwaka 2015” amesema Dk. Tizeba.

Amesema, malengo mengine ya mageuzi hayo ni kuhakikisha taifa linajitosheleza kwa chakula ikiwa ni pamoja na kujenga mfumo imara wa hifadhi ya chakula kitaifa na ugavi ili kuruhusu ubobevu.

Lengo lingine ni kuongeza uzalishaji na tija ya kilimo, hasa kwa mazao ya biashara na mazao ghafi kwa uzalishaji viwandani ili kuchochea uwekezaji katika mnyororo wa thamani wa uzalishaji wa mazao hayo kuendeshwa kibiashara.

“Mageuzi hayo yatatusaidia kuongeza uwezo kama nchi wa kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi ambayo yamekuwa na athari sana kwenye kilimo nchini” amesema Waziri Tizeba.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

TCRA yatoa leseni 224 za watoa huduma za maudhui mtandaoni…93 ni za Blogs, 97 ni za Online Tv.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba amesema leseni 224 zimetolewa kwa watoa huduma

Read More...

Muungano wa Afrika umeiomba DR Congo uahirishe kutangaza matokeo kamili ya uchaguzi mkuu

Muungano wa Afrika (AU) umeitaka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo iahirishe kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu. Muungano huo unaonuia

Read More...

Bunge kupiga kura tena 29 mwezi januari.

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ataitisha kura nyingine Januari 29 kuhusu makubaliano ya Uingereza kujitoa kutoka Umoja wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu