Serikali imenunua na kusambaza vifaa vya maabara vyenye thamani ya Sh bilioni 16 ili kuboresha ufundishaji wa masomo ya sayansi kwa vitendo.

In Kitaifa

Serikali imenunua na kusambaza vifaa vya maabara vyenye thamani ya Sh bilioni 16 ili kuboresha ufundishaji wa masomo ya sayansi kwa vitendo.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Selemani Jafo alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Grace Tengega (CCM).

Tengega alitaka kujua serikali ina mpango mkakati gani wa kuboresha zana za kufundishia ili kwenda sambamba na ukuzaji wa ujuzi wa stadi za taaluma wanazosoma.

Amesema usambazaji wa vitabu hivyo, umeboresha uwiano wa kitabu kwa mwanafunzi kutoka uwiano wa 3:1 hadi 1:2 lengo ni kufikia uwiano 1:1 kwa kuzingatia Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015.

Aidha, katika kuboresha elimu nchini, serikali imeanza kutoa posho kila mwezi kama motisha kwa walimu wakuu, wakuu wa shule na waratibu elimu kata ili kuimarisha uongozi na usimamizi wa elimu.

Aidha, serikali kupitia ofisi ya Rais-Manejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, inafanya mapitio ya majukumu ya watumishi wote wakiwemo walimu ili kuboresha maslahi ya watumishi kwa kuzingatia uzito wa kazi.

Ametoa rai kwa viongozi wote wakiwamo wabunge katika maeneo yao, kubuni utaratibu wa kuwapa motisha watumishi ili kuwapa ari ya kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

 

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu