Serikali imerejea kauli yake ya kuhakikisha watu wanaofanya mauaji ya polisi na viongozi wa Chama cha Mapinduzi katika wilaya za Kibiti na Rufiji Mkoani Pwani wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

In Kitaifa

Serikali imerejea kauli yake ya kuhakikisha watu wanaofanya mauaji ya polisi na viongozi wa Chama cha Mapinduzi katika wilaya za Kibiti na Rufiji Mkoani Pwani wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Mwigulu Nchemba amesisitiza kuwa operesheni maalum inayoendelea katika wilaya hizo ni lazima itoe matokeo yatakayomhakikishia kila mwananchi maisha salama ndani ya nchi hii.

Ametoa kauli hiyo wakati alipofanya ziara ya kukagua kambi maalum ya operesheni ya kuwatafuta wauaji wa baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi wilayani Kibiti, akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoani Pwani ambaye pia ni mkuu wa Mkoa huo Mhandisi Evarist Ndikilo.

Katika maelezo yake, Waziri huyo wa mambo ya ndani amesema hisia zilizokuwepo kwamba pengine mauaji hayo yanahusishwa na katazo la biashara ya mazao ya misitu ukiwemo mkaa, misimamo ya kidini, Ujambazi ama ugaidi siyo za kweli, bali ni mchezo uliobuniwa na kundi la watu kwa sababu ambazo haziko wazi na kwa hiyo ni lazima vitendo hivyo vikomeshwe mara moja.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu