Serikali imesema itaanza kuwatambua wazalishaji wadogo wa umeme na kuwasimamia, hata kama wanazalisha umeme kwa kiasi kidogo .
Hayo yamesemwa jijini Dodma Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani ,wakati wa kikao baina yake na watumishi wa Tanesco na wa mradi wa umeme vijijini REA.
Dkt.Kalemani amesema kuwa ni wajibu wa Tanesco na REA kuwatambua wazalishaji wadogo wa umeme, ifike mahali ufanyike utafiti unaoweza kusaidia kuongeza umeme, na wale wenye leseni za EWURA.
Aidha amesema kuwa watendaji hao wameitwa ili kutafakari walichokifanya 2018/2019, na kujipanga upya kutekeleza majukumu yao katika mwaka wa fedha unaoanza julai ili kuhakikisha huduma zinakuwa imara muda wote.
Aidha amewataka kusimamia suala la kupeleka umeme kwenye taasisi kama vyuo, shule, makanisa, hospitali na taasisi nyingine ,zikaweze kusaidia jamii ya maeneo husika.
Waziri Kalemani ametaja baadhi ya ajenda moja wapo Iliyojadiliwa katika kikao hicho, ni utekelezaji wa kupeleka umeme vijijini kwa nchi nzima.