Serikali yaipongeza Ubungo kwa kufanikisha Mikopo kwa Wanawake walemavu na Vijana

In Kitaifa

Leo tarehe 30 April 2018, Serikali kupitia Naibu waziri wa OFISI YA RAIS TAMISEMI ,Ndugu Joseph KakundaKakunda amei Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa kuwa Halamshauri ya Kwanza na Ya Mfano kwa kutoa Fedha za Mikopo ya Wanawake na Vijana kwa asilimia 100,kutoka katika Mapato ya Ndani.

Mhe. Naibu Waziri ameitaka Wizara ya TAMISEMI kuandikia Manispaa ya Ubungo Barua Ya Pongezi ,kwaku jambo hilo limekuwa gumu sehemu Nyingi Sana, na wengine kutenga fedha chache sana Tofauti na Manispaa ya Ubungo ambao leo wamezindua Zoezi la Ugawaji wa Mikopo ya kiasi cha Tsh Billion 1.94,wakati ina Mwaka Mmoja tu Tangu kuanzishwa kwake.

Naye Mstahiki Meya Boniface Jacob,amesisitiza kuwa mikopo itatolewa kwa Vigezo bila kuangalia dini,kabila wala chama cha mtu,na “Waaosema Mikopo ni ilani ya CCM,wajiulize mbona kwingine kuna Halmashauri za CCM lakini hakuna mambo haya mazuri? Hivyo watu wajue viongozi Makini na Imara wanatoka Chama cha Upinzani ndiyo Msingi na Chachu ya Mafanikio yetu”

Akisoma Hotuba kwa Mgeni Rasmi Mkurugenzi Kayombo,amesema leo Halmashauri imeidhinisha Kutoa fedha kwa Vikundi 364 ambapo vikundi 119 ni vya Vijana na Vikundi 245 ni vya wanawake,ambapo jumla watakao nufaika na Mikopo ni wananchi 11,312.

MWISHO
Mstahiki Meya Ametoa rai kwa Vijana kujitokeza zaidi kuomba mikopo hiyo,kwakuwa idadi ya akina Mama ni Kubwa Ziaidi kiliko Vijana,huku akihaidi mwezi ujao Halmashauri kuanzisha Viwanda vidogo kwa ajili ya kuwasaidia Vijana suala la ajira.

Imetolewa na
Ofisi ya Mstahiki Meya
Manispaa ya Ubungo
30 April 2018

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu