Serikali yakanusha tuhuma za ubaguzi mikopo vyuoni.

In Kitaifa

Serikali imekanusha kuhusu tuhuma za kwenye sera ya elimu ya mwaka 2014 kuwa ni ya kibaguzi kwa wanafunzi nchini hasa kwa wale wanaosoma kwenye shule za binafsi na kusema kuwa yote wanayofanya ikiwepo kutotoa mikopo kwa wanafunzi wote ni kutokana na ufinyu wa bajeti.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea kuhusu vigezo vinavyotumika na serikali kuwanyima mkopo wanafunzi waliosoma shule za binafsi, huku akieleza kuwa sera ya elimu imefanya ubaguzi.

“Tunachoangalia ni nani mwenye uhitaji zaidi, sio suala la kibaguzi, bajeti ni iliyopo ndogo wahitaji ni wengi. Kwa wanafunzi waliopata bahati ya kusomeshwa na wafadhili shule binafsi serikali haiwanyimi mikopo tutahitaji ushahidi kweli walifadhiliwa”. – William Ole Nash

Aidha Mhe. Ole Nasha ameongeza “Kuhusu watoto ambao wamesoma shule binafsi kutoruhusiwa kupata mikopo ni suala la kuangalia kati ya mtu ambaye ameweza kulipa milioni 3 au 4 ya shule ya msingi na sekondari na yule ambaye hakuweza, ni yupi utampa kipaumbele kupata mkopo, sio tunabagua”.- William Ole Nasha

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu