Serikali Yakataa Kuivunja Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW).

In Kitaifa

Semio Sonyo (News Room)

Serikali imesema iko tayari kupokea ushauri wa namna bora yakuimarisha utendaji wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa kuwa azma ya Serikali ni kuendeleza Taasisi hiyo kwani bado inahitajika na madhumuni ya kuanzishwa kwake  yana  tija kwa Taifa.
Akizungumza wakati akijibu Hoja za Wabunge na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma  na Maendeleo ya Jamii Waziri wa Elimu Sayansi na Teknplojia Profesa Joyce Ndalichako amesema kuwa Bado Taasisi hiyo inahitajika hivyo Serikali inaangalia namna ya kuiboresha na si kuivunja kama ilivyopendekezwa.
“ Taasisi ya Elimu ilianzishwa kwa lengo la kutoa elimu kwa wale waliokosa katika mfumo rasmi na pia kutoa mafunzo  endelevu hivyo bado kuna umuhimu wa kuendeleza Taasisi hii” Alisisitiza Prof. Ndalichako.
Akifafanua  Prof. Ndalichako amesema kuwa Taasisi hiyo inaweza kuimarishwa zaidi ili  kuendana na mahitaji ya sasa  ikiwa ni sehemu ya mikakati ya Serikali kuimarisha na kukuza kiwango cha elimu nchini.
Akizungumzia mikakati yakuimarisha elimu nchini Profesa Ndalichako amesema kuwa kwa sasa Serikali inafanya ukarabati wa Shule Kongwe hapa nchini, vyuo vya Ualimu, na Ujenzi wa maktaba yakisasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam  yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 2500 kwa wakati mmoja hiyo ikiwa ni sehemu ya miradi yakuboresha elimu inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii yalipendekeza kuwa TEWW ivunjwe ambapo Serikali imesema kuwa Bado Taasisi hiyo inahitajika na ina tija hivyo kitakachofanyika ni kuiboresha zaidi ili kukuza elimu hapa nchini na Si kuivunja kama ilivyopendekezwa.
Taasisi hiyo imeanzishwa kwa sheria namba 139 ya mwaka 1989 na iko chini ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Suzan Kiwanga afukuzwa Bungeni.

Spika wa Bunge, Job Ndugai jana alimtoa nje ya bunge, Mbunge wa Mlimba, Suzan Kiwanga (Chadema) na kumtaka kutohudhuria

Read More...

Mtolea ajivua Uanachama wa CUF Akiwa Ndani ya Bunge Leo.

Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea, kwa tiketi ya CUF ametangaza kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge na nafasi zote ndani

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu