Serikali yamkana Nabii Tito.

In Kitaifa
Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Sheria wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Marlin Komba amesema hamtambui  mtu anayejiita nabii Tito na kwamba hajasajili kanisa lake katika ofisi ya msajili wa taasisi za dini.
Komba amesema Serikali imeona vitendo anavyovifanya ‘nabii’ huyo kupitia mitandao ya kijamii na imeanza kuchukua hatua.
“Ninachoweza kusema ni kwamba hakuna mtu anayezuiwa kuongea hapa nchini, mwache aongee anavyoweza ila Serikali imeshaona anachokifanya na yanayoendelea mitandaoni  hatua zinachukuliwa dhidi yake,” amesema Komba.
Kwa upande wao viongozi wa dini wameonyeshwa kukerwa na kulaani vitendo anavyovifanya mtu huyo anayejiita nabii na kusisitiza kuwa hakuna dini inayoruhusu hayo.
Msaidizi wa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Mchungaji Chediel Lwiza amesema kwa vitendo anavyofanya mtu huyo hapaswi kujiita mtumishi wa Mungu.
“Huyo hawezi kuwa mtumishi wa Mungu na wala hafanyi huduma ya kanisa ni vyema watu kama hawa wafuatiliwe na hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao. Natumaini Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo ndani yake ina ofisi ya msajili wa taasisi za dini itafanya kazi yake.”
Lwiza ametumia fursa hiyo kuwasisitiza Watanzania kwenda kwenye makanisa ya kweli yanayozingatia neno la Mungu.
Amesema, “Hakuna sababu ya kutangatanga, Watanzania mkasali kwenye makanisa yanayotambulika na yanayosimamia na kufundisha neno la Mungu. Kuhangaika ndiko kunakowafanya wengine waangukie kwa watu kama hao. Wapo wanaojaribu kupotosha neno la Mungu lakini ukweli ni kwamba neno la Mungu halipotoshwi.”

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu