Zaidi ya shilingi bilion 2.8 zimetolewa na serikali kwa ajili ya ujenzi wa shule ya secondary ya elimu maalumu katika eneo la chuo cha Pandandi kilichopo Tengeru wilaya ya Arumeru mkoani Arusha
Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya miundombinu wilayani Arumeru Mkuu wa wilaya hiyo Mh, Jery Muro amesema kuwa fursa hiyo ni ya kwanza hapa nchini ambapo italeta manufaa kwa watu wenye mahitaji maalumu
Amesema kuwa licha ya kusaidia kitaleta kielelezo cha kuhakikisha watoto wenye ulemavu watapewa mtazamo mpya wa elimu kwa kuokoa watoto wenye changamoto na mahitaji maalumu kutoka sehemu mbalimbali
insert gambo,,,,,
Aidha ameseama kila mwezi serikali inatoa bilioni 23 kwa wastani kwa ajili ya ujenzi wa elimu na kugharamia sera ya elimu bure hapa nchini
Kwa upande wake Mkuu wa shule ya mahitaji maalumu Patandi Mwl. Janeth Molel ameipongeza serikali kwa juhudi kubwa za kuwajali watu wenye mahitaji maalumu hasa kupitia elimu kwani hii itasaidia kupunguza ongezeko la watoto wa mtaani na hatiamye kufikia malengo ya Tanzania ya viwanda
Amsesema kuwa,kwa sasa yamekamilika madarasa manane 8 na itachukua wanafunzi wenye mahitaji maalumu ambapo tayari wameshapata waalimu 5 kwa ajili ya kuanza kutoa elimu hiyo ambayo itakuwa shule ya mfano hapa Tanzania