Serikali yatoa onyo kwa watumishi wa umma wanaotoa siri za serikali.

In Kitaifa

Serikali imetoa onyo kwa watumishi wa umma wanaotoa siri za serikali na kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii kuwa watachukuliwa hatua za kisheria.

Onyo hilo limetolewa jijini Dar es Salaam  na Waziri wa Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki wakati wa ufunguzi wa mkutano wa watumishi wa umma wa Manispaa ya Ubungo.

Kairuki amesema mtumishi wa umma atayejihusisha na usambazaji wa taarifa za serikali, atachukuliwa hatua za kisheria ikiwamo kufikishwa mahakamani na kupewa kifungo cha miaka 20 jela.

Aidha amefafanua kuwa serikali ina utaratibu wake wa kutoa taarifa kwa umma ikiwa ni pamoja na kupitia machapisho yake kwa jamii.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu