Shahidi akwama kutokea Mahakamani kesi ya Mdee.

In Kitaifa

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa ahirisho la mwisho kwa upande wa mashtaka katika kesi ya kutumia lugha ya matusi dhidi ya Rais John Magufuli inayomkabili Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kwa sababu wameshindwa kufika na shahidi.

Hayo yamesemwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya Wakili wa serikali Mwandamizi, Patrick Mwita kudai kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

Wakili Mwita amedai kuwa hawana shahidi na kwamba hiyo ni mara ya tatu hawana shahidi, hivyo wanaomba ahirisho.

Kutokana na hatua hiyo, Hakimu Simba amesema anatoa ahirisho la mwisho kwa upande wa mashtaka, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi June 29,2018.

Katika kesi hiyo Mdee anadaiwa kuwa alifanya kosa hilo July 3,2017 katika Makao Makuu ya Ofisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) iliyopo mtaa wa Ufipa wilaya ya Kinondoni.

Anadaiwa  kumtukana Rais John Magufuli  kuwa “anaongea hovyohovyo,anatakiwa  afungwe breki” kitendo ambacho kingeweza  kusababisha uvunjifu wa Amani.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Azam yapoteza mbele ya ndanda

MOHAMED Mkopi wa Ndanda FC alipachika bao dakika ya 62 lililomshinda mlinda mlango wa Azam FC, limevunja mwiko wa

Read More...

CAF YAWAPIGA CHINI MAREFA WA TANZANIA AFCON 2019, YACHUKUA HADI WA BURUNDI,KENYA,TANZANIA HOLAA.

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya marefa 27 na marefa wasaidizi 29 kwa ajili ya Fainali za

Read More...

Man U, Juventus wafungishwa virago UEFA

Timu ya Manchester United imeondoshwa katika michuano ya ligi ya mabingwa ulaya hatua ya robo fainali baada ya kukubali

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu