SIELEWI NINI KINAENDELEA KATI YA MCHUMBA WANGU NA RAFIKI YANGU, NAOMBENI USHAURI

In Mahusiano

Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 27, nafanya kazi katika Company moja ya simu, nina mchumba
wangu ambae tumekuwa na uhusiano wa miaka minne sasa, nateyari ameshanivalisha pete, kwao
nafahamika nae kwetu anafahamika, lakini siku za hapa karibuni nimekuwa siwaelewi yeye na rafiki
yangu mimi, nina huyu rafiki yangu ambae nampenda sana, na namshirikisha mambo mengi, hadi kwa
mchumba wangu nimemtambulisha na anamfahamu vizuri, miezi miwili iliyo pita mchumba wangu
alikuwa na graduation, Basi kwakuwa aliniambia baada ya kutoka chuoni kutakuwa na part ya
kumpongeza mahali fulani, basi nami sikusita kumfata rafiki yangu kumualika, cha ajabu nilipokuwa
nikimuelezea alidakia na kunieleza kila kitu, kwamba mbona shem alishaniambia, siku nyinigi? wakat
mimi ndio nimetoka kuambiwa, iliniuma lakini nilitake easy, basi ikafika siku ya tukio, nikampitia rafiki
yangu kwao, sikumkuta isipokuwa nilikuta wadogo zake na nikakuta box kubwa sana la zawadi,
nilipouliza wakasema amefunga zawadi ametoka kidogo, wewe tangulia tu! tukafika ukumbini, tumekaa
kidogo nae rafiki yangu akaingia akiwa na box lake la zawadi, kitu nilichonote pale nikwamba rafiki yangu
na mchumba wangu walikuwa wamebadilika sana, kila mtu ananijibu dry kwa chochote nitakachouliza,
nikawa nimekosa amani kabisa, kabla ya party kuisha nilitangulia kwenye gari ya mchumba wangu,
nikaanza kulia, sababu sikuwa nikijisikia vizuri, party ilipoisha walikuja hadi kwenye gari, mchumba
wangu na rafiki yangu, akaniambia, kwanini uko huku? nikamwambia najisikia vibaya, wala hakuonyesha
kujali, akaniuliza tunaenda wote nyumbani? nikamwambia ndio, akasema ngoja tukamshushe kwanza
rafiki yako kwao ndio twende, nikamwambia sawa, bas hata wakati tuko kwenye gari, walikuwa wakipiga
story wao, mimi wamenitenga kabisa, hata wakiongea nikichangia wanapotezea ile mada na kuleta

ingine, inaniuma sana, kwani nampenda sana mchumba wangu, tulipomfikisha kwao tukarudi kwa
mchumba wangu, tukaanza kufungua zawadi, nilikuwa nina hamu ya kujua ndani ya box la rafiki yangu
kuna nini, nilipofungua sikutaka kuamini nilichokiona, nikakuta amemuwekea chupi za dazani moja, boxer
dazani moja, kondom box zima, vest, viwembe, tauro,na mashuka, na picha yake, nikamuuliza mchumba
wangu, imekuwaje? akasema unaniuliza mimi? muulize rafiki yako, nililia sana, nikampigia rafiki yangu
simu, cha ajabu hakuonyesha kushtuka kabisa, ndio kwanza akaanza kucheka akasema mimi nilifikiri
umekuta bastola au bomu, kumbe umekuta zawadi za kawaida tu! niache nilale bwana, akakata simu,
nilitoka usiku uleule hadi nyumbani, nilililia sana, kesho yake nikawanampigia simu mchumba wangu
akawa hapokei na hata rafiki yangu pia akawa hapokei,  nikaenda nyumbani kwa wazazi wa mchumba
wangu nikawaeleza wakakasirika sana, wakamuita, walimsema na pale pale baba yake akamuuliza
unampango gani na binti wa watu, jibu hapahapa, yeye akasema ananipenda na bado anataka kunioa,
lakini toka tutoke kwenye kikao kile, nimekuwa simuelewi kabisa, ananishushua hovyo, ananikaripia tu

hata mbele za watu, hataki kutoka na mimi kama zamani,

hali hii inanipa shida sana, nashindwa hata kufanya kazi zangu kwa ufanisi, inaniuma sana yani. naomba
mnisaidie dada violet na wadau wengine, nimepoteza muelekeo wa maisha kabisa,

bado nampenda sana mchumba wangu,

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu