Uongozi wa Simba umesema kuwa mpango mkubwa kwenye
mchezo wao wa kimataifa wa kirafiki kilele cha Simba day
ilikuwa kucheza na waarabu wa Misri, timu ya Al Ahly ila
imeshindikana kutokana na janga la Virusi vya Corona.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Agosti 19, Ofisa
Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa mipango yao
ilikwama kutokana na uwepo wa janga la Corona ambalo
limevuruga ratiba nyingi duniani
Mchezo huo unatarajiwa kuanza majira ya saa 10 jioni na
milango Uwanja wa Mkapa kutakakochezwa mchezo huo na ule
Uwanja wa Uhuru ambapo kutakuwa na ‘Big Screen’
itafunguliwa majira ya saa mbili asubuhi.
