Serikali Wilayani Serengeti Mkoani Mara imekiri kuwepo kwa
kundi la Simba linaloendelea kula mifugo ya wananchi katika
wilaya hiyo ambapo mpaka sasa ng’ombe zaidi ya 70
wameuawa na Simba hao huku mbuzi na kondoo wakifikia 40.
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara Mh Nurdin Babu
tayari amewasiliana na Mkurugenzi wa wanyama pori kuagalia
namna ya kuwapa wananchi waliokubwa na mkasa wa kuliwa
kwa mifugo yao kupata kifuta machozi.