Simba yawatambia Mwadui

In Michezo

Afisa habari wa Simba Haji Manara amesema kuelekea mchezo wa Ligi kuu soka Tanzania bara leo Juni 20, 2020, kati ya Simba dhidi ya Mwadui FC, hawatarajii kama kutakuwa na matokeo matatu.

Kupitia taarifa aliyotuma kwa vyombo vya Habari, amesema wanachojua wao ni ushindi tu hivyo Mwadui watawasamehe kwa hilo.

”Mwadui tunawaheshimu sana walitufunga mechi ya kwanza na pia tuliwafunga kwa taabu sana kwenye hatua ya mtoano ya Kombe la shirikisho, lakini ni lazima wajue pointi tatu tunazihitaji hivyo tupo tayari kwa hilo”, amesema Manara.

Aidha Manara amesema mchezo utapigwa Saa 10:00 jioni kwenye uwanja wa taifa, tofauti na ambavyo imekuwa ikielezwa kuwa utapigwa Saa 11:00 jioni.

Simba inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na pointi 72 katika mechi 29, wakati Mwadui FC ina pointi 34 katika mechi 29 ikiwa katika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tetesi za soka Ulaya.

Inter Milan wanafikiria kumnunua kiungo wa kati, Mfaransa N'Golo Kante huku Blues wakiwa tayari kusikiliza ofa kwa ajili

Read More...

Manchester City kushiriki kombe la Ulaya.

Klabu ya Manchester imefanikiwa kubadili marufuku ya miaka miwili kushiriki katika mashindano ya klabu bingwa Ulaya kuanzia msimu

Read More...

Mama akiri kuua Watoto wake wanne.

Mwanamke mmoja nchini Kenya Betrice Mwende, anayeshikiliwa kwa tuhuma za kuwaua watoto wake wanne, amekiri Mahakamani kuwa ni

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu