SOKA LA KIMATAIFA NA FUNUNU ZAKE.

In Michezo

Klabu ya Real Madrid itawapasa watoe kitita cha euro milioni 80 wakitaka kumfuta kazi kocha wao Zinedine Zidane. Zidane amekuwa kwenye shinikizo kubwa kutokana na timu hiyo kutofanya vizuri. (Sport)

Barcelona sasa ni klabu kubwa nyengine inayotajwa kumnyemelea mshambuliaji kinda Erling Braut Haaland, 19, wa klabu ya Red Bull Salzburg. Raia huyo wa Norway alikuwa mwiba mkali kwa klabu ya KRC Genk (inayochezewa na Mtanzania Mbwana Samatta) kwa kufumania nyavu zao mara tatu siku ya Jumanne. (Mundo Deportivo)

Baba wa Haaland, Alf-Inge, ameweka wazi kuwa itakuwa “vizuri” endapo mwanawe atajiunga na Manchester United, licha ya baba mtu kuchezea klabu hasimu za Leeds na Manchester City katika enzi zake. (TV2 kupitia Mail)

Klabu ya Liverpool imeanza mazungumzo ya kumuongezea mkataba wa miaka mitano unusu mshambuliaji wake rai wa Senegal Sadio Mane, 27. Mkataba huo utamfanya Mane awe mchezaji anayelipwa vizuri zaidi Anfield kwa kitita cha pauni 220,000 kwa wiki. (Gazzetta dello Sport kupitia Star)

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

TUME YA MADINI KWENYE MKUTANO WA KIMATAIFA WA MADINI

Kamishna wa Tume ya Madini, Profesa Abdulkarim Mruma akielezea fursa zilizopo kwenye Sekta ya Madini Tanzania katika

Read More...

Halmashauri ya Jiji la Arusha kutokomeza mimba za utotoni.

Halmashauri ya Jiji la Arusha ikishirikiana na wataalamu wa Afya kutoka mashirika mbalimbali, maafisa  elimu kata na sekondari,

Read More...

MNADA WA ALMASI WDL WAZIDI KUPAMBA MOTO.

Leo tarehe 20 Februari, 2020 mnada wa asilimia tano ya madini ya almasi kutoka katika Mgodi wa Williamson Diamond

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu