Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) Patrick Ole Sosopi ameitaka tume ya uchaguzi kusimamia uchaguzi wa jimbo la uchaguzi kuwa wa huru na haki katika jimbo la Monduli ili wananchi waweze kupata viongozi bora kupitia uchaguzi unazingatia sheria ,kanuni na misingi ya demokrasia.
Akizungumza na Wanahabari katika Ofisi za CHADEMA Wilayani hapo ambapo amesema kuwa iwapo sheria na kanuni zitaheshimiwa wataweza kuibuka na ushindi katika jimbo hilo kwani wana mgombea anayekubalika na wananchi.
Patrick amesema kuwa tayari wamejiandaa kufanya kampeni za kistaarabu katika vijiji vyote vilivyopo katika wilaya hiyo na kumnadi mgombea wao.
Mgombea wa kiti cha Ubunge kupitia chama hicho Yonas Laizer amesema kuwa baada ya uteuzi katika chama chake tayari wananchi wameonesha nia ya kumchagua hivyo anaamini ataibuka na ushindi katika uchaguzi huo.