Sugu, Masonga waachiwa kwa dhamana

In Kitaifa
Mahakama ya Hakimu Mkazi-Mbeya imewaachia kwa dhamana washtakiwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga katika kesi inayowakabili ya kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.
Sugu na Masonga wamekaa mahabusu kwa muda wa siku 24 baada ya kunyimwa dhamana na mahakama hiyo kutokana na hoja za upande wa  Jamhuri.
Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Michael Mteite amewaachia kwa dhamana wawili baada ya Wakili upande wa utetezi, Peter Kibatala kuiambia mahakama hiyo kwamba imeshafunga ushahidi wake ambapo mashahidi sita walitoa ushahidi wao.
Mawakili wa pande zote mbili walikubaliana kwamba Februari 19 watawasilisha majumuisho ya shauri hilo mahakamani hapo.
Hakimu Mteite amekubaliana  na hoja hiyo ya mawakili na kusema hukumu ya kesi hiyo itatolewa Februari26 mwaka huu.
“Washtakiwa wote wanaachiwa kwa dhamana, na kila mmoja atajidhamini mwenyewe kwa hati ya dhamana ya maneno ya Sh5 milioni kwa kila mmoja.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Museveni akanusha kupigwa vibaya Bobi Wine.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekanusha kwamba mbunge wa upinzani Bobi Wine amejeruhiwa. Katika taarifa yake ya kwanza kuhusu

Read More...

Dada yake Rais Magufuli aaga dunia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefiwa na dada yake, Monica Joseph Magufuli aliyekuwa amelazwa katika

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu