Tahadhari Ya Mvua Kubwa toka TMA.

In Kitaifa
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari ya vipindi  vya mvua kubwa vinavyotarajiwa katika msimu wa Novemba 2018 hadi Aprili 2019 katika kanda za magharibi, kati na nyanda za juu kusini.
Maeneo yatakayoathirika na mvua hizo za juu ya wastani hadi wastani ni Dodoma, Singida, Tabora, Mbeya, Njombe, Iringa, Ruvuma, Kusini mwa Morogoro, Lindi na Mtwara.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Oktoba 18, 2018 Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agness Kijazi amesema  utabiri huo ni kwa mikoa inayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka.
“Katika kipindi cha mvua za msimu hali ya unyevunyevu wa udongo kwa ustawi wa mazao na upatikanaji wa chakula cha samaki vinatarajiwa kuimarika katika maeneo mengi,” amesema.
“Hata hivyo, mazao yasiyohitaji maji mengi kama vile mahindi, maharage na mtama yanaweza kuathiriwa na hali ya unyevunyevu wa kupitiliza na maji kutuama.”
Kutokana na mvua hizo, Kijazi amewatahadharisha pia wachimbaji wa madini hasa wadogo kuwa makini na ongezeko la maji linaloweza kusababisha mmomonyoko wa ardhi au maji kujaa kwenye mashimo.
Pia, amezishauri mamlaka za miji na majiji kuchukua tafadhali kwa kuhakikisha mifumo ya kupitisha maji inafanya kazi ili kuepusha maji kutuama na kusababisha mafuriko yanayogharimu maisha ya watu na uharibifu wa miundombinu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu