TAIFA STARS YAIPIGA CHINI HARAMBEE STARS CHAN..

In Michezo

TIMU ya soka ya Taifa, Taifa Stars imesonga mbele kwenye michuano ya kuwania kufuzu fainali za kombe la mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani, Chan baada ya
kuifunga Kenya kwa mikwaju ya penalti 4-1 katika mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Mosi Kasarani Nairobi.
Fainali za Chan zimepangwa kufanyika Cameroon mwakani na Stars inawania kufuzu fainali hizo kwa mara ya kwanza baada ya miaka 10.

Timu hizo zililazimika kwenda kwenye mikwaju ya penalti baada ya mechi hiyo kumalizika kwa suluhu matokeo ambayo pia yalipatikana katika mechi ya kwanza
iliyochezwa uwanja wa Taifa wiki moja iliyopita.
Shujaa wa Stars jana alikuwa kipa mkongwe Juma Kaseja aliyepangua penalti moja kati ya mbili walizokosa Kenya.
Mechi hiyo ilikuwa ya vuta nikuvute kwa muda wote huku Stars ikitaka kushinda ili kulipa kisasi katika mechi ya makundi ya Afcon Misri baada ya kufungwa mabao 3-2 na
Kenya.

Katika mechi hiyo, wachezaji wa Taifa Stars iliyo chini ya kocha wa muda Etiene Ndayiragije walionyesha ukakamavu mkubwa katika muda wote wa mtanange huo.
Ushindi huo unaifanya Stars sasa kucheza na Sudan Septemba mwaka huu na ikishinda itaingia hatua ya makundi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

SOKA LA KIMATAIFA NA FUNUNU ZAKE

Real Madrid bado wanataka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazili Neymar, lakini wanataka hakikisho kutoka Paris St-Germain kuhusu hali

Read More...

(TAMISEMI) KUTOA TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani S Jafo kesho tarehe 23 Mwezi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu