(TAKUKURU) Dodoma yabaini viashiria vya rushwa katika mradi wa ujenzi wa shule wenye thamani ya sh. milioni 471

In Kitaifa

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Dodoma inachunguza miradi miwili ya ujenzi wa shule za sekondari yenye thamani ya sh. milioni 471 baada ya kubainika kuwa na viashiria vya rushwa.

Kadhalika, inamshikiria mwanafunzi wa Chuo cha St. John mkoani hapa kwa kosa la kutoa hongo ya sh. 900,000 kwa Ofisa Mitihani chuoni hapo ili aongeze alama za ufaulu kwa wanafunzi wenzake sita.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, Mkuu wa TAKUKURU mkoani Dodoma, Sothenes Kibwengo, alisema miradi hiyo ya ujenzi wa shule imeonekana kuwa na udanganyifu.

“Kuanzia Oktoba hadi Desemba mwaka jana, tulikagua miradi kwenye sekta ya elimu kubaini iwapo thamani halisi ya fedha ilifikiwa. Miradi miwili ya ujenzi katika shule za sekondari yenye thamani y ash. milioni 471 imeonekana na viashiria vya udanganyifu,” alieleza.

Kibwengo alisema udanganyifu huo umebainika katika matumizi ya fedha, hivyo uchunguzi unafanyika kubaini kama kuna jinai.

Akizungumzia kukamatwa kwa mwanafunzi wa chuo cha St. John, mkuu huyo wa TAKUKURU Dodoma alisema mwanafunzi huyo James Kwangulija alitoa hongo ya sh. laki tisa kwa Ofisa Mitihani wa chuo hicho.

“Alijaribu kutoa hongo ili asaidiwe kuongeza alama za ufaulu kwa wanafunzi wenzake sita, kinyume na kifungu cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, sura ya 329 marejeo ya mwaka 2018,” alieleza.

Alitoa wito kwa wananchi kujiepusha na vitendo vya rushwa huku akiomba wananchi waendelee kutoa taarifa za vitendo hivyo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Mwenyekiti Bavicha taifa aomba udhamini ubunge.

Mwenyekiti wa Vijana Taifa chama cha Chadema John Pambalu amejitokeza kutia nia na kuomba udhamini kwa wanachama wa chama hicho katika

Read More...

RC Makonda amkaribisha DC Gondwe

Mkuu wa Mkoa DSM wa Paul Makonda leo July 9 amezungumza na Mkuu wa Wilaya mpya wa Temeke Mh Godwin Gondwe pamoja

Read More...

Takukuru Dodoma watoa kauli kuhusu mbunge kibajaji.

Kufuatia kuwepo kwa taarifa za TAKUKURU mkoani Dodoma kumshikilia mbunge wa Jimbo la Mtera Ndugu Livinstone Lusinde Kibabaji, leo wamezungumzia swala hilo. Kwa uzuri Mtaa wa Mastory

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu