TAKUKURU yawafikisha mahakamani wafanyabiashara James Rugemarila na Habinder Sethi.

In Kitaifa

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)  imewafikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wafanyabiashara James Rugemarila na Habinder Sethi, kwa tuhuma za uhujumu uchumi na makosa mengine yanayofanana na hao.

Hayo yamesemwa  na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Valentino Mlowola alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa muda mrefu wamekuwa wakiulizwa kuhusu kesi ya Escrow hivyo sasa anaamini ni wakati muafaka wa kuwafikisha watuhumiwa hao wawili mahakamani.

Mlowola amesema kuwa taasisi hiyo imefanya uchunguzi wa kutosha kwa muda wote ambao ilikuwa kimya, na hivyo wamefikishwa mahakamani kisutu, baada ya hapo mahakama itafanya taratibu za kuhamishia kesi hiyo katika Mahakama ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Kabla ya vigogo hawa wawili kufikishwa mahakamani hapo jana, baadhi ya watumishi wa TANESCO tayari walishtakiwa kufuatia tuhuma za kupokea fedha kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya VIP Engeneering & Marketing ,ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa kampuni ya kufua umeme ya Independent Power Tanzania Ltd (IPTL), James Rugemalira.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu