Tambwe: Yanga tupo imara.

In Michezo

MSHAMBULIAJI wa timu ya Yanga, Amiss Tambwe amesema kuwa kikosi cha Yanga ni imara na kinauwezo wa kushindana na timu yoyote ndani na nje ya Tanzania kama ilivyo Simba.

Tambwe ambaye amecheza timu zote mbili kubwa za bongo, ambao ni Simba na Yanga mpaka sasa amepachika mabao 72 kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kutua bongo.

“Yanga ni timu imara na ina uwezo wa kushindana na timu nyingi hapa bongo na nje ya bongo, kwa kuwa tumecheza mechi nyingi za kimataifa hali inayotufanya tuwe imara kwenye ushindani.

“Kwa sasa ni suala la mpito tu ambalo tunalipitia ila bado wachezaji tunafanya vizuri hata ukitazama mpaka sasa tumepambana na tumejikusanyia pointi 80 kwenye ligi si haba, hata wapinzani wetu Simba nao wapo vizuri isipokuwa tunapishana vitu vidogo tu na ndio maana tunashindana nao,” amesema Tambwe.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

SOKA LA KIMATAIFA NA FUNUNU ZAKE

Real Madrid bado wanataka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazili Neymar, lakini wanataka hakikisho kutoka Paris St-Germain kuhusu hali

Read More...

(TAMISEMI) KUTOA TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani S Jafo kesho tarehe 23 Mwezi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu