TANESCO WAHAMIA DODOMA

In Kitaifa

MKURUGENZI Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Dk Tito Mwinuka amezindua rasmi ofisi mpya ya Dodoma na kubainisha kuwa makao makuu ya shirika hilo
sasa yamehamia rasmi Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokewa katika osi za Tanesco, Dk Mwinuka alisema kuanzia sasa shughuli zote zitafanyika kuanzia Dodoma na
huduma zote za kiofisi zitaendelea kama kawaida katika kanda saba, mikoa 29 ya Kitanesco na Wilayani.
Alisema uwepo wa serikali Dodoma huku makao makuu ya Shirika hilo yakiwa Jijini Dar es Salaam ufanisi wa kazi unaweza kuwa si mzuri. “Tukiwa Dodoma ufanisi wetu
utakuwa ni mzuri, natumaini tutatoa huduma bora zaidi kwa wananchi,” alisema.
Alisema ujio wa serikali Dodoma utasababisha ujenzi wa majengo mengi yakiwemo ya serikali na huduma ya umeme itahitajika sana. Dk Mwinuka alisema katika awamu
ya kwanza, watumishi 30 wameshaka Dodoma kutoka makao makuu Dar es Salaam. “Tutajenga jengo jipya hapa Dodoma ambalo litawapokea watu wote watahaohamia
Dodoma,” alisema.

Alisema jengo hilo jipya litajengwa na bajeti yake itatengwa mwaka ujao wa fedha na sasa kinachofanyika ni matayarisho ya mwanzo fedha zitakapokuja. Wakati huo huo,
Waziri wa Nchi Osi ya Makamu wa Rais – Mazingira na Muungano, January Makamba jana alikagua eneo litakapojengwa osi za wizara hizo huku akibainisha kuwa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar itakuwa na ofsi zake kwenye makao makuu ya serikali. Akizungumza katika mji wa serikali eneo la Mtumba alisema ofsi yake ina ekari
nane kwa ajili ya ujenzi wa ofisi.

Alisema wataanza na ujenzi wa jengo dogo la muda ili likikamilika watumishi wahamie. “Rais ametoa fedha kwa kila Wizara, tuko kwenye mchakato kwa kumpata mjenzi,
ikiwemo wakala wa serikali na vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo Suma JKT,” alisema.
Alisema Ofisi ya Makamu wa Rais ni ofisi ya pili kubwa kiserikali lazima waoneshe dhamira ya kuhamia haraka Dodoma na kutakuwa na mpango wa kupendezesha
mazingira katika mji wa serikali.

“Sisi tunasimamia Muungano ushiriki wa Zanzibar utakuwepo na kutokana na hilo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imepata ekari 10 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi
zake. Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Joseph Malongo alisema michoro ya jengo hilo imetayarishwa na Wakala wa Majengo (TBA) na jengo la chini
litakuwa na mita za mraba 1,050.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Baraka da Prince sasa kufunga ndoa na Naj

Msanii wa Bongo fleva Baraka de Prince amebainsha wazi kufunga ndoa mwaka huu na mpenzi wake Naj. Minong’ono ilikua

Read More...

Ajibuawataka Simba watulize boli, msimu ni wao

Nyota wa Simba, Ibrahim Ajibu amesema kuwa mashabiki wa Simba watulie watakubali mziki wake kwani amejipanga kufanya maajabu. Ajibu

Read More...

Waziri Mkuu kuzindua Daftari la kudumu la kupiga kura.

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Dkt Athumani Kihamia, amesema zoezi la uandikishaji wa daftari la Kupiga

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu