TANZANIA NA MALAWI YAINGIA MAKUBALIANO

In Kitaifa

Tanzania na Malawi zimekubaliana kushirikiana kuboresha sekta za usafirishaji, uvuvi, madini, nishati, utalii na kilimo.
Makubaliano hayo yalitangazwa jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa hafla maalum iliyohusisha marais wa nchi hizo mbili, mwenyeji Dk. John Magufuli na Rais Lazarus Chakwera aliyezuru nchini kwa ziara ya siku tatu.

Rais Magufuli alimshukuru Rais Chakwera kwa kuitembelea Tanzania na kuwa nchi ya tatu kutembelewa barani Afrika kwa kiongozi mpya wa Malawi baada ya Burundi na Uganda tangu aingie madarakani.

Katika hafla hiyo, Rais Magufuli alisema nchi hizo mbili zina historia ya undugu kutokana na mwingiliano wa watu wake katika shughuli mbalimbali ikiwamo biashara.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yakanusha Madai ya kuwepo kwa vituo na wapigakura hewa

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imewataka wanasiasa na wagombea wanaodai kuwepo kwa vituo na wapigakura hewa kupeleka

Read More...

Leteni Mbunge Wa Kupitisha Bajeti, Siyo Wa Kupinga Tu – Majaliwa

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu