Tanzania yang’ara urusi.

In Michezo

Timu ya Wasichana ya Tanzania inayoundwa na Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu wa Kituo cha TSC Mwanza wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya Kombe la Dunia la Watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu baada ya kuifunga Uingereza magoli 2-1.

Mchezo huo uliyopigwa kwenye dimba la klabu ya Lokomotive mjini Moscow nchini Urusi Tanzania iliibuka na ushindi huo mnono kupitia kwa wachezaji wake, Mastura Fadhili na Mshambuliaji Asha Omari.

Kwa upande mwingine timu ya Brazili imetinga hatua ya fainali baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1 – 0 dhidi ya  Ufilipino.

Tanzania ambayo ndiyo mabingwa watetezi baada ya kulitwaa kombe hilo mwaka 2014, itaikabili Brazil kwenye mchezo wa fainali unaotarajiwa kupigwa kesho kutwa huku mpaka sasa ikiwa imeruhusu wavu wake kutikiswa mara moja tu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Museveni akanusha kupigwa vibaya Bobi Wine.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amekanusha kwamba mbunge wa upinzani Bobi Wine amejeruhiwa. Katika taarifa yake ya kwanza kuhusu

Read More...

Dada yake Rais Magufuli aaga dunia.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amefiwa na dada yake, Monica Joseph Magufuli aliyekuwa amelazwa katika

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu