Tanzania yapata tuzo.

In Afya, Kitaifa

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeipa tuzo Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya katika jitihada zake za kupambana na ugonjwa wa malaria.

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Muhammed Bakari (kulia) akipokea cheti cha kutambua mchango mkubwa uliofanywa na Serikali ya Tanzania katika kupambana na ugonjwa wa Malaria kutoka kwa mwakilishi wa WHO nchini Dkt. Ritha Njau .

Akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kupokea tuzo hiyo jana Jumatatu Februari 26, 2018, Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohammed Bakari amesema matukio ya wagonjwa wanaougua malaria yamepungua kwa kiasi kikubwa.

“Kumekuwa na mafanikio kwa maana ya mwaka 2008 kwa matukio ya wagonjwa wa malaria ambayo yaliripotiwa yalikuwa milioni 18, mwaka 2017 namba hiyo imepungua na kuwa ni milioni 5.5, haya ni mafanikio makubwa sana katika udhibiti wa malaria nchini,” amesema Prof. Bakari.

Kwa upande mwingine Bakari amesema kudhibiti malaria kwa watoto wa chini ya miaka mitano ni mafanikio makubwa kwa sekta ya afya nchini.

“Takwimu za mwaka 2008 zinaonyesha kuwa vifo vya watoto chini ya miaka mitano vilikuwa ni 112 kati ya watoto 1,000 na mwaka 2017 tunaona vifo vimepungua mpaka kufikia 67 kwa watoto 1,000, hii inaonyesha mafanikio makubwa katika maendeleo ya kudhibiti malaria,” amesema Prof Bakari.

Aidha, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la WHO nchini, Dkt. Rita Njau amesema tuzo hiyo imetolewa kwa Tanzania baada ya kufanikiwa kupunguza maambukizi ya malaria kwa kipindi cha miaka 10.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Baraka da Prince sasa kufunga ndoa na Naj

Msanii wa Bongo fleva Baraka de Prince amebainsha wazi kufunga ndoa mwaka huu na mpenzi wake Naj. Minong’ono ilikua

Read More...

Ajibuawataka Simba watulize boli, msimu ni wao

Nyota wa Simba, Ibrahim Ajibu amesema kuwa mashabiki wa Simba watulie watakubali mziki wake kwani amejipanga kufanya maajabu. Ajibu

Read More...

Waziri Mkuu kuzindua Daftari la kudumu la kupiga kura.

Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Dkt Athumani Kihamia, amesema zoezi la uandikishaji wa daftari la Kupiga

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu