Tanzia: Baba mzazi wa Mama Salma Kikwete afariki dunia.

In Kitaifa

Mke wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum (CCM) amepata pigo kwa kuondokewa na baba yake mzazi, Mzee Rashid Mkwachu jana Julai 19, 2018.

Akitoa taarifa hiyo kwa niaba ya familia, Ridhiwani Kikwete amesema kuwa Mzee Rashid amefariki leo na shughuli za mazishi zitakuwa Msasani nyumbani kwa Dkt. Kikwete.

Ridhiwani pia ameeleza kuwa mazishi yatafanyika katika makaburi ya Kisutu saa kumi jioni baada ya sala ya alasiri.

“Kwa niaba ya Familia ya Mama Salma Rashid-Kikwete na Dr. Jakaya Kikwete, naomba kutoa taarifa kuwa Mama Salma Rashid Kikwete amefiwa na Baba yake Mzazi Mzee Rashid Mkwachu.”

Radio 5 tunatoa pole kwa wafiwa wote na Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali Pema Peponi, Amen.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu