Tanzia:Sam wa Ukweli afariki Dunia.

In Burudani
Msanii  wa Bongo Fleva, Sam wa Ukweli amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Palestina iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu na mwili wake umehifadhiwa katika Hospital ya Mwananyamala.
Taarifa hiyo imethibitishwa na msambazaji wa nyimbo zake ambaye pia Meneja wa ‘Team Mtaa kwa Mtaa’, Amri the Business aliyeeleza kwa masikitiko alivyopokea makubwa kuwa Sam amefariki dunia na kumtakia kupumzika kwa amani.
“Siamini kilichotokea muda huu ila sina jinsi, kwani woote safari ni moja, pumzika kwa amani Sam wa Ukweli, hakika nilikupenda kama ndugu yangu wakuzaliwa tumbo moja, #rip” amesema Amri the Business.
Aidha, aliyekuwa mtayarishaji wa nyimbo za Sam wa Ukweli, Producer Steve amesema Sam alizidiwa zaidi Jumamosi iliyopita na walipomuuliza alisema ni ‘UKIMWI wa kulogwa’.
Sam wa Ukweli aliwahi kutamba na ngoma kama Sina Raha, Hata Kwetu Wapo, Sisikii, Milele na nyingine nyingi kali kuanzia mwaka 2010

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu