Tetesi za soka Ulaya

In Kimataifa, Michezo

Mustakabali wa Jordan Henderson, 31 katika klabu ya Liverpool haueleweki, mazungumzo ya mkataba mpya wa kiungo huyo wa England yameshindwa kuendelea tangu kumalizika kwa msimu. (The Athletic – subscription required)

Chelsea inafahamu kiungo wa England na West Ham United Declan Rice, 22, ana nia ya kujiunga nao na watawasiliana na wagonga nyundo hao kujua nini cha kufanya ili kukamilisha mpango huo. (Express)

Declan Rice on England duty
Maelezo ya picha,Declan Rice

Manchester City wanamtaka beki wa kushoto wa Sporting Lisbon na Ureno Nuno Mendes, 19, lakini hawako tayari kutoa kitita cha £50m inayotakiwa na wareno hao. (Fabrizio Romano)

Atletico Madrid wanaendelea na msimamo wao kwamba beki wake raia wa England Kieran Trippier, 30, hauzwi licha ya Manchester United kuonyesha nia ya kumtaka- lakini klabu hiyo ya Hispania huenda ikamsajili beki wa kulia wa Wolves na Ureno Nelson Semedo, 27, au beki wa kulia wa Napoli na Italia Giovanni di Lorenzo, 27, iwapo Trippier ataamua kuondoka. (AS)

Tottenham Hotspur wako katika mazungumzo mazuri na Atalanta kuhusu uhamisho wa beki wa kati wa Argentina Cristian Romero, 23. (Football.London)

Manuel Locatelli
Maelezo ya picha,Manuel Locatelli

Arsenal mpaka sasa wako kando katika harakati zao za kumshawishi kiungo wa Italia Manuel Locatelli, licha ya utayari wao wa kulipa dau la £34m wanalolitaka Sassuolo – huku nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 akijiandaa kuichagua Juventus kutokana na kushiriki kwakwe kwneye michuano ya klabu bingwa Ulaya. (Mirror)

Beki wa kati wa Real Madrid na Ufaransa Raphael Varane, 28, yuko tayari kutua ligi kuu ya England huku Manchester United wakiwa na imani kubwa kwamba, kuhusu mshahara na marupurupu yake haitakuwa tatizo. (Guardian)

Varane
Maelezo ya picha,Varane

United wanakaribia kukamilisha uhamisho wa Varane. (MEN)

Barcelona wamepewa fursa ya kumsajili kiungo wa Manchester United na Uholanzi Donny van de Beek, 24, wakati Klabu hiyo ya Hispania pia ikimtumia beki wake mfaransa Samuel Umtiti, 27, kama sehemu ya mpango huo. (Sport via Express)

Kwingineko, Mmiliki wa Napoli Aurelio de Laurentiis amekataa dau la £30m lililotolewa na Manchester United kwa ajili ya mlinzi wa klabu hiyo Kalidou Koulibaly, 30. (Gazzetta)

Kuli
Maelezo ya picha,Kalidou Koulibaly

United wako tayari kuvuta subira katika harakati zao za kumshawishi kiungo wa Rennes mfaransa Eduardo Camavinga, 18, wakati huu wanapojaribu kupunguza dau lake. (The Athletic – subscription required)

Kiungo wa United, mfaransa Paul Pogba, 28, mshambuliaji wa Juventus na Ureno Cristiano Ronaldo, 36, na mshambuliaji wa Paris St-Germain, mfaransa Kylian Mbappe, 22, ni miongoni mwa wachezaji wanaoweza kuwa huru msimu ujao, kutokana na athari za janga la corona zilizozikumba klabu zao. (ESPN)

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Hukumu ya Bernard Morrison kutolewa leo

Kesi inayomuhusisha aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Yanga ambaye kwa hivi sasa anakipiga Simba Sc, Bernard Morrison itasikilizwa na

Read More...

Kamanda wa AFRICOM azuru Tanzania akiangazia ushirikiano katika nyanja ya usalama

Kamanda wa Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani (AFRICOM) Jenerali Stephen Townsend, alikuwa na ziara ya siku

Read More...

TETESI ZA SOKA ULAYA

Paris St-Germain imeanza mazugumzo ya awali na Paul Pogba kuangalia kama anaweza kujiunga nao kutoka Manchester United msimu huu

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu