TETESI ZA SOKA ULAYA

In Kimataifa, Michezo

Paris St-Germain imeanza mazugumzo ya awali na Paul Pogba kuangalia kama anaweza kujiunga nao kutoka Manchester United msimu huu ama msimu ujao, wakati kiungo huyo mfaransa mwenye umri wa miaka 28, atakapokuwa mchezaji huru. (Athletic, subscription required)

United wako tayari kupokea ofa kutoka PSG na wanataka dau la angalau £45m kwa ajili ya Pogba. (Eurosport)

Arsenal wamemuweka beki wa kulia wa kihispania Hector Bellerin, 26, katika mpango wa kubadilishana na mshambuliaji wa Inter Milan, Muargentina Lautaro Martinez, 23. (Football Insider)

Aston Villa imetoa £25.5m kwa ajili ya Leon Bailey, 23, lakini Bayer Leverkusen inataka £29.8m kwa ajili ya winga huyo Mjamaica, ambaye anawawindwa pia na vilabu vya Leicester City na Wolves. (Bild – in German)

Tottenham wanamuwania Dusan Vlahovic kutaka Fiorentina, ambao huenda wakahitaji dau la £50m kwa ajili ya mshambuliaji huyo wa Serbia mwenye umri wa miaka 21. (Telegraph)

halaand

Mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 21, na winga wa Ujerumani Julian Brandt, 25, watasalia Borussia Dortmund msimu huu. (Tuttosport – in Italian)

Ajax imethibitisha kwamba vilabu vya Arsenal na Lyon vimeonyesha nia ya kutaka kumsajili mlinda mlango wake raia wa Cameroon Andre Onana, 25 ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa kwa sababu ya dawa za kusisimua misuli. (Voetbal International, via Sun)

Norwich City wanajiandaa kutoa kitita cha £10m kwa ajili ya kumsajili winga wa PAOK Salonika, mgiriki Christos Tzolis mweye umri wa miaka 19. (Football Insider)

Barcelona bado hawajakubaliana mkataba mpya na Ilaix Moriba, kinda wa kihipsania mwenye umri wa miaka 18, ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao na tayari vilabu kadhaa vya ligi kuu ya England vimeonyesha nia ya kumtaka. (Marca)

Aston Villa itamruhusu winga wa kiholanzi Anwar El Ghazi, 26, kuondoka kwa ada ya £15m kama Roma watapekeka ofa kufuatia kuonyesha nia ya kumtaka. (Football Insider)

loca

Juventus wanakutana tena na maafisa wa Sassuolo wakiwa na matumaini ya kukamilisha mpango wa kumsajili kiungo wa kimataifa wa Italia Manuel Locatelli, 23, na wanataka pia kumsajili mshambuliaji wa kibrazili Kaio Jorge, 19, kutoka Santos. (Tuttosport – in Italian)

Crystal Palace, Newcastle na Monaco ni miongoni mwa vilabu vinavyomtaka kiungo wa zamani wa timu ya taifa ya vijana ya Ufaransa chini ya miaka 21 kutoka Angers Angelo Fulgini, 24. (Mail)

Mpango wa Manchester United wa kumsajili kiungo wa Ureno kutoka Wolves Ruben Neves, 24, uko mbali kabisa na kukamilika. (Eurosport, via Express)

toby

Tottenham walimuuza mlinzi Toby Alderweireld kwenda Al-Duhail ya Qatari kwa ada ya £3m ingawa alikuwa na mkataba wa mpaka mwaka 2023 na akiwa na miaka 32 tu. (Sun)

Leeds United wameambiwa wanapaswa kutoa £5m kama wanataka kumsajili mlinzi wa kushoto wa Hibernian raia wa Scotland Josh Doig, 19 msimu huu. (Leeds Live)

Liverpool imepoteza mamilioni ya pauni baada ya mlinzi wa kushoto Yasser Larouci, 20 mualgeria kuondoka bure kwenda Troyes. (Mirror)

Ethan Ennis amefanya mazungumzo na Chelsea msimu huu, lakini kiungo huyo mwenye umri wa miaka 16 amechagua kujiunga na Manchester United baada ya kukataa mkataba mpya wa kusalia Liverpool. (Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa Ubelgiji Aaron Leya Iseka, 23, anajiandaa kujiunga na Barnsley ya Championship kutoka Toulouse baada ya msimu uliopita kucheza kwa mkopo Metz. (L’Equipe – in French)

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tetesi za Soka Ulaya leo Alhamisi Septemba 23, 2021

Mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette, 30, hana hamu ya kusaini kandarasi mpya klabuni hapo. Mkataba wake wa

Read More...

Wanaharakati wa haki za binadamu wahoji hukumu dhidi ya Rusesabagina

 Makundi ya kutetea haki za binadamu barani Afrika yamelalamikia uamuzi wa mahakama kuu ya Rwanda ya kumfunga jela kwa miaka 25, Paul Rusesabagina ambaye alisifika sana kwenye filamu ya Hollywood ya Hotel Rwanda.  Mahakama hiyo Jumatatu ilisema kwamba imepata Rusesabagina pamoja na washukiwa wengine 20 na hatia ya

Read More...

LISSU NA WENZAKE WAFUTIWA KESI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeifutia kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleao

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu