Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 06.05.2021: Konate, Salah, Conte, Lamela, Mata, Williams

In Kitaifa, Michezo

Chelsea itapambana na Manchester City katika fainali ya Ligi ya Mabingwa huko Istanbul baada ya kuishinda Real Madrid mabao mawili kwa nunge huko Stamford Bridge.

Chelsea ilistahili ushindi huo ambao utafanikisha fainali ya vilabu viwili vya ligi kuu ya Uingereza dhidi ya vijana Pep Guardiola mnamo 29 Mei baada ya ushindi wao wa jumla ya mabao matatu kwa moja baada ya mikondo yote miwili.

m

Liverpool wamekubaliana kuhusu masharti binafsi na kiungo wa kati wa Ufaransa na RB Leipzig Ibrahima Konate, 21, anayejiandaa kujiunga na klabu ya primia kwa mkataba wa miaka mitano. (Talk Sport)

West Ham imejiunga na Chelsea na vilabu vingine katika mbio za kumnasa mshambuliaji wa Brentford Ivan Toney, 25, ambaye ana gharama ya pauni milioni 35. (Sun)

Mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah anataka kuondoka Liverpool na Paris St-Germain wanapanga kumpata mchezaji huyo ,28, ikiwa mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe,22, ataondoka majira ya joto. (Le Parisien-in French)

m

Wakati huo huo, PSG wanatafuta kuimarisha safu ya ulinzi na wamebainisha kuwa mlinzi wa kulia wa Tottenham na Ivory Coast Serge Aurier,28, kuwa ni lengo lao muhimu. (RMC Sport in French)

Norwich City wako kwenye mchuano na Southampton na West Ham kumnasa mchezaji wa nafasi ya ulinzi kinda Brandon Williams,20, kwa mkopo anayekipiga Manchester United. (Sun)

Tottenham imefanya mazungumzo na kocha wa Inter Milan Antonio Conte kuhusu nafasi iliyo wazi ndani ya Spurs. Mazungumzo na Muitaliano huyo, 51 yamekuja baada ya Conte kuiwezesha Inter kutwaa taji lao la kwanza baada ya miaka 11. (Corriere dello Sport,via Express)

sport

Jose Mourinho anaweza kumtaka nahodha wa zamani Daniele De Rossi,37, kuungana naye kama kocha msaidizi atakapochukua nafasi ya kocha wa AS Roma msimu ujao. (Calciomercato-in Italian)

Kocha wa zamani wa Spurs Mourinho atatazama uwezekano wa kumsajili kiungo wa kati wa Tottenham Erik Lamela,29, na mshambuliaji wa Brazil Lucas Moura,28. (Football.London)

Vinginevyo, Mourinho atatafuta wachezaji wawili wa Spurs Muingereza Eric Dier, 27, na Dane Pierre-Emile Hojbjerg, 25, pamoja na mchezaji wa Uhispania wa Manchester United Juan Mata, 33. (Corriere dello Sport)

Hwang Hee-chan,
Maelezo ya picha,Hwang Hee-chan

West Ham na Crystal Palace wanafuatilia uhamisho wa mshambuliaji wa RB Leipzig na Korea Kusini Hwang Hee-chan,25. (Telegraph)

Uimara wa mshambuliaji wa Brazil Wesley,24, ambaye hivi karibuni alirejea baada ya kuwa benchi kwa karibu miezi 16 kutokana na jeraha kubwa la mguu, kutategemea kama Aston Villa watamsajili mshambuliaji mwingine. (Express &Star)

Benfica na RB Leipzig wanamfuatilia kwa karibu kiungo wa kati wa Leicester City Sidnei Taraves, lakini klabu yake ina mpango wa kumpatia mkatava mpya mchezaji huyo wa Ureno mwenye miaka 19. (Football Insider)

m

Leeds United imeibuka kama mshindani wa “ghafla” kusaini kiungo wa Uturuki mwenye umri wa miaka 26 Ozan Tufan kutoka Fenerbahce, ambaye hapo awali alikuwa akihusishwa sana na taarifa za kuelekea Uhispania. (Fotomac-in Turkish)

Lazio inafikiria kumpatia mkataba wa miaka miwili kiungo wa kati wa Manchester United Juam Mata baada ya wakala wa mchezaji huyo,33,kuwasiliana na klabu hiyo kuhusu masuala ya uhamisho. (II Tmpo-in Italian)

Atletico Madrid inataka kumsajili kiungo wa kati wa Argentina anayekipiga CA Colon Facundo Farias,18, ambaye ana thamani ya uhamisho ya pauni milioni 9 kwa mujibu wa kipengele cha mkataba wake na klabu hiyo ya Argentina. (AS-in Spanish)

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

SABAYA AFIKISHWA MAHAKAMANI

Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake 5 wafikishwa mahakamani kwa makosa matano ikiwemo

Read More...

George Mkuchika Aaapishwa kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais Ikulu, Kazi Maalum.

Rais Samia Suluhu Hassan amemuapisha Kampeni Mstaafu George Mkuchika kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais Ikulu, Kazi Maalum. Kabla ya

Read More...

Waziri wa Uganda ajeruhiwa na mwanae kufa baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana

Watu wenye silaha wamemshambulia na kumjeruhi Waziri na Kamanda wa zamani wa jeshi la Uganda, na kumuua binti yake

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu