Tetesi za soka Ulaya Jumatano 10.03.2021

In Kimataifa, Michezo

Manchester United itasikiliza ofa za kumuuza kipa wake David De Gea mwisho wa msimu huu huku mkufunzi Ole Gunnar Solskjaer akiwa tayari kumfanya Dean Anderson kuchukua nafasi ya kwanza ya mlinda lango.. (90min via Mail)

Hatahivyo klabu hiyo inamnyatia kipa wa Atletico Madrid na Slovenia Jan Oblak, 28. (Sky Sports)

Arsenal imeripotiwa kwamba iko tayari kuchukua fursa ya mzozo unaoendelea katika klabu ya Inter Milan kwa kuwasilisha ofa ya kumnunua beki wa Morocco Achraf Hakimi. (Mirror)

Achraf Hakimi
Maelezo ya picha,Achraf Hakimi

Manchester United na Manchester City zinafikiria kumsajili beki wa Villareal na Uhispania Pau Torres, 24. (Manchester Evening News)

Crystal Palace inapanga uhamisho wa kiungo wa kati wa Sheffield United John Lundstram, 27, na mwenzake wa Chelsea Conor Gallagher, 21, huku wakijiandaa kubadilisha kikosi hicho mwisho wa msimu huu. (Express)

Kiungo wa kati wa Schalke na Uhispania Omar Mascarell, 28, ameonekana kama mchezaji anayelengwa na klabu ya Wolves mwisho wa msimu huu. (Caught Offside)

Omar Mascarelli
Maelezo ya picha,Omar Mascarelli

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anatumai anaweza kumshawishi mshambuliaji wa Sergio Aguero, 32, kusalia na klabu hiyo zaidi ya msimu. (Star)

Real Madrid ina hamu ya kumsaini winga wa Manchester City na Algeria Riyad Mahrez, 30. (FootMercato – in French)

Beki wa kati wa Celtic na Uskochi Jack Hendry, 25, ameripotiwa kunyatiwa na klabu ya Aston Villa, kwa dau la £10m mwisho wa msimu. (Birmingham Mail)

Barcelona imeafikia makubaliano ya maneno na klabu ya Bayern kumnunua beki wa Austria na Bayern Munich David Alaba, 28. (Mundo Deportivo – in Spanish)

David Alaba

Inter Milan imewasiliana na ajenti wa beki wa Ufaransa na Real Betis Aissa Mandi, 29, ambaye alikuwa analengwa na Liverpool mwezi Januari. (Calciomercato – in Italian)

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Rais Samia Suluhu Hassan atuma salamu za mfungo wa Ramadhani

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewatakia Waislamu wote mfungo mwema wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.Rais Samia Suluhu Hassan,

Read More...

Mourinho alia na VAR kisa kiwiko cha Pogba

Kocha Mkuu wa Tottenham, Jose Mourinho anaamini kwamba kiungo wa Klabu ya Manchester United, Paul Pogba alistahili kuonyeshwa kadi

Read More...

Namungo FC yarejea Bongo tayari kwa ligi kuu bara

Kikosi cha Namungo FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Moroco leo Aprili 12 kimerejea Tanzania kikitokea nchini Zambia ili

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu