Tetesi za Soka Ulaya leo Ijumaa Septemba 10, 2021

In Kimataifa, Michezo

Chelsea wamepanga kufufua ari yao kumsajili beki wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22 Jules Kounde wakati wa dirisha la uhamisho la Januari ikiwa Sevilla itapunguza gharama yake kwa karibu euro 50m (ESPN)

Blues, pamoja na Paris St-Germain na Liverpool, pia zinasemekana kumtaka Kiungo wa kati wa AC Milan na Ivory Coast Franck Kessie, 24. (Calciomercato – in Italian)

Arsenal wameripotiwa kumtambua mshambuliaji wa Sevilla Youssef En-Nesyri, 24, kama mbadala bora wa muda mrefu wa mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 32, lakini raia huyo wa Morocco ameazimia kukaa katika kilabu hiyo ya Uhispania. (La Colina de Nervion – in Spanish)

Winga wa Bayern Munich Kingsley Coman huenda akakataa ofa zozote kutoka kwa mabingwa wa Bundesliga kuongeza mkataba wake kwani mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 “anaota” kuhamia Ligi ya Premia. (Le10Sport – in French)

Kiungo wa Ubelgiji, Youri Tielemans anatazamwa na Real Madrid, Barcelona na Manchester United wakati Leicester ikijaribu kumfunga nyota huyo wa miaka 24 kwa mkataba mpya. (AS – in Spanish)

The Foxes pia wamewasiliana na Sassuolo ya Serie A kuhusu winga wa Italia Domenico Berardi, 27, juu ya uwezekano wa uhamisho mwezi Januari (Leicester Mercury)

ny

Barcelona ilitoa ofa ya pauni milioni 68 kumsajili tena mshambuliaji Neymar, 29, kabla ya ukweli wa shida za kifedha za kilabu hiyo kushuhudia Lionel Messi akihama na kujiunga na Mbrazil huko Paris St-Germain (Star)

Liverpool itamlenga kiungo wa Valencia na Uhispania Carlos Soler, 24, kama mbadala wa Mholanzi Georginio Wijnaldum, 30, ambaye aliondoka kujiunga na PSG msimu huu wa joto. (Fichajes – in Spanish)

Kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba anadhani meneja Ole Gunnar Solskjaer anapaswa kumsajili kiungo wa Ufaransa anayekadiriwa kwa thamani ya juu sana Monaco Aurelien Tchouameni, 21 (Express)

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta anafurahi Ainsley Maitland-Niles anasalia na Gunners, na alifichua kuwa alifanya mazungumzo ya faragha na kijana huyo wa miaka 22 baada ya kiungo huyo wa England kuelezea hadharani hamu ya kuondoka klabuni hapo majira ya joto (Mirror)

th

Arteta amedokeza kiungo wa Uingereza Jack Wilshere, 29, anaweza kufanya mazoezi na kilabu yake hiyo ya zamani Arsenal wakati anajaribu kupata kilabu mpya kufuatia kuachiliwa kwake kutoka Bournemouth.(Mirror)

Everton ilijaribu kukubali makubaliano na timu ya Uturuki Istanbul Basaksehir kumuuza kiungo James Rodriguez, 30, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia alikataa kuondoka Goodison Park(AS – in Spanish)

Rais wa Barcelona Joan Laporta amethibitisha mkutano umepangwa na maajenti wa Ousmane Dembele, 24, wakati kilabu kilabu hiyo inapopanga kumpa Mfaransa huyo mkataba mpya. . (Fabrizio Romano)

AC Milan wana nia ya kumsajili winga wa Real Madrid na Uhispania Marco Asensio, 25, msimu ujao wa joto (TDFichajes – in Spanish)

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tetesi za Soka Ulaya leo Alhamisi Septemba 23, 2021

Mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette, 30, hana hamu ya kusaini kandarasi mpya klabuni hapo. Mkataba wake wa

Read More...

Wanaharakati wa haki za binadamu wahoji hukumu dhidi ya Rusesabagina

 Makundi ya kutetea haki za binadamu barani Afrika yamelalamikia uamuzi wa mahakama kuu ya Rwanda ya kumfunga jela kwa miaka 25, Paul Rusesabagina ambaye alisifika sana kwenye filamu ya Hollywood ya Hotel Rwanda.  Mahakama hiyo Jumatatu ilisema kwamba imepata Rusesabagina pamoja na washukiwa wengine 20 na hatia ya

Read More...

LISSU NA WENZAKE WAFUTIWA KESI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeifutia kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleao

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu