TETESI ZA SOKA

In Michezo

Barcelona wanakaribia kufikia mkataba wa kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, lakini uhamisho wa bure wa kiungo huyo aliye na umri wa miaka 32- utategemea ikiwa klabu hiyo ya Nou Camp itafanikiwa kumshawishi mshambuliaji mwenzake wa Argetina Lionel Messi, 33, kusalia nao. (AS)

Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer huenda akawauza wachezaji Jesse Lingard, 28, Juan Mata,32, Diogo Dalot 21 na Phil Jones, 29, kuongezea bajeti yake ya £80m msimu wa joto. (Metro)

Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund Michael Zorc, amesema klabu hiyo imepatia kipaumbele kushinda Ligi ya Mabingwa kupitia Bundesliga wanapojitahidi kusalia na mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland, 20, kwa “muda mrefu iwezekanavyo”. (Welt an Sonntag, via Goal)

mshambuliaji wa Norway Erling Braut Haaland
Maelezo ya picha,Mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland

Manchester City wamewasiliana na Sporting Lisbon kumhusu mlinzi wao Nuno Mendes wanapojiandaa kuitangulia Real Madrid katika juhudi za kumsajili nyota huyo Mreno aliye na umri wa miaka 18. (AS, via Mail)

Arsenal wanamtaka mlinzi wa Eintracht Frankfurt Mfaransa Evan N’Dicka, 21, na wameomba kupewa maelezo kuhusu hali ya kiungo wa kati wa Brighton na Mali Yves Bissouma,24. (Express)

Lautaro Martinez
Maelezo ya picha,Mshambuliaji wa Inter Milan Lautaro Martinez, 23, anaamini kuwa atasaini mkataba mpya na klabu hiyo

Mshambuliaji wa Inter Milan Lautaro Martinez, 23, anaamini kuwa atasaini mkataba mpya na klabu hiyo, licha ya kile Muargentina huyo alichotaja kuwa “changamoto kidogo za kifedha” zunazokabili klabu hiyo ya Italia. (Sky Sports Italia, via Goal)

Christian Eriksen alikuwa amehusishwa na tetesi za kuondoka Inter Milan mwezi Januari lakini nyota huyo mwenye umri wa miaka 29- anasema anafurahi kuwa katika klabu hiyo ya Serie A. (Sky Sports Italia, via Football Italia)

Christian Eriksen

Chelsea inahitaji angalau euro milioni 20 kumpata mlinzi wa Italia Emerson Palmieri,26, lakini Inter Milan na Napoli pia zinataka kumsajili. (Calciomercato, via Football Italia)

Tetesi za Soka Jumapili

Kocha wa Juventus Andrea Pirlo amesema ni “kawaida kuwepo kwa uvumi” wa hatma ya mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo katika klabu hiyo baada ya kutoka kwenye Ligi ya Mabingwa lakini mchezaji huyo, 36, “amekuwa na mchezo mzuri” kwa timu hiyo ya Serie A. (Football Italia)

Ronaldo
Maelezo ya picha,Kocha wa Juventus Andrea Pirlo amesema ni “kawaida kuwepo kwa uvumi” kuhusu hatma ya Ronaldo

Ronaldo, ambaye amehusishwa na kurejea Real Madrid, amesema kuwa alichokipa kipaumbele sasa hivi ni kumaliza msimu kwa kishindo na Juventus. (Mail on Sunday)

Manchester United iko tayari kutoa mkataba mpya kwa Ole Gunner Solskjaer kwasababu wa sasa hivi unakamilika baadaye mwezi huu. (Sunday Mirror)

Edinson Cavani
Maelezo ya picha,mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani yuko katika hatari ya kupigwa kalamu Manchester United

Solskjaer atafanya mazungumzo ya uhamisho na timu ya Manchester United – huku mshambuliaji wa Uruguay Edinson Cavani, 34, Mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 25, na mlindalango wa Uhispania David de Gea, 30, wakiwa katika hatari ya kupigwa kalamu. (Sun on Sunday)

Barcelona inataka kumuuza mchezaji wa Brazil Philippe Coutinho, 28, ili iweze kulipa Liverpool deni lililosalia kutoka uhamisho wake wa mwaka 2018. (Sport – in Spanish)

Barcelona inataka kumuuza mchezaji wa Brazil Philippe Coutinho
Maelezo ya picha,Barcelona inataka kumuuza mchezaji wa Brazil Philippe Coutinho

Mkataba wa kiungo wa kati wa Liverpool Georginio Wijnaldum na klabu yake unamalizika msimu huu na makubaliano ya mchezaji huyo, 30, wa Uholanzi kuhamia Barcelona yamefikiwa kwa asilimia “95”. (Football Insider)

Paul Pogba wa Manchester United yuko kwenye orodha ya waliolengwa wakati wa uhamisho na Paris St-Germain klabu hiyo ya Ligue 1 imewasiliana na kiungo huyo wa kati, 27, raia wa Ufaransa. (Foot Mercato – in French)

Manchester United wamemuongeza mlinda lango wa Burnley Nick Pope katika orodha yao ya uhamisho, ingawa huenda ikakabiliwa na ushindani kutoka Tottenham Hotspur kwa mchezaji huyo, 28, wa England. (Star on Sunday)

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

SABAYA AFIKISHWA MAHAKAMANI

Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake 5 wafikishwa mahakamani kwa makosa matano ikiwemo

Read More...

George Mkuchika Aaapishwa kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais Ikulu, Kazi Maalum.

Rais Samia Suluhu Hassan amemuapisha Kampeni Mstaafu George Mkuchika kuwa Waziri katika Ofisi ya Rais Ikulu, Kazi Maalum. Kabla ya

Read More...

Waziri wa Uganda ajeruhiwa na mwanae kufa baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana

Watu wenye silaha wamemshambulia na kumjeruhi Waziri na Kamanda wa zamani wa jeshi la Uganda, na kumuua binti yake

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu