Theresa May aishutumu Urusi kuhusika kumshambulia Sergei Skripal.

In Kimataifa

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May amasema kuwa serikali yake ina amini kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa Urusi imehusika katika shambulio la mpelelezi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal na mtoto wake wa kike, lilitokea kusini mwa Uingereza katika mji wa Salisbury.

Aidha Bi May ameongeza pia inawezekana tukio hilo limelengwa moja kwa moja na Urusi dhidi ya Uingereza ama Urusi imeshindwa kudhibiti kemikali zake hatari.

”kuna mambo mawili tu yanaweza kuhusika kwa shambulio lilotokea, inawezekana serikali ya Urusi ilikusudia kufanya tukio hili hapa Uingereza, ama imeshindwa kudhibiti silaha hizi hatari za kemikali na hivyo imesababisha imetumiwa na watu wengine” Alisema May.

Sergei Skripal(kulia) na binti yake bado wapo mahututi hospitalini
Sergei Skripal(kulia) na binti yake bado wapo mahututi hospitalini

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson ameunga mkono Uingereza kwa kusema kuwa huenda Urusi inahusika moja kwa moja katika shambulio hilo, kwa upande wake msemaji wa ikulu ya white house Sarah Sanders ametoa pole na kwa raia wa Uingereza bila kuunga mkono shutuma ya Uingereza kwa Urusi.

kwa upande wake mbunge kutoka chama tawala nchini Urusi , Vitaly Milonov amesema kuwa shambulio hilo dhidi ya mpelelezi wa zamani ni mbinu iliyotumika kuihusisha Urusi na si vinginevyo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Kitambulisho cha Vladimir Putin cha ujasusi chapatikana Ujerumani.

Kitambulisho cha Vladimir Putin alichopewa kama jasusi Ujerumani alipokuwa anafanya kazi kama jasusi wa Urusi kimepatikana katika makavazi mjini

Read More...

May aairisha kura kuhusu Brexit.

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ameahirisha kura iliyokuwa ifanyike leo bungeni kuhusu makubaliano ambayo serikali yake na Umoja

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu