Timu ya wasichana U-17 yarejea nchi na ubingwa COSAFA

In Michezo

Kikosi cha timu ya Taifa ya Wasichana chini ya umri wa miaka 17 ‘Tanzanite Queens’ kimetua hapa nchini usiku wa kuamkia leo wakitokea nchini Afrika Kusini ambapo walifanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika (COSAFA).

Tanzania ilitwaa ubingwa huo baada ya kuwafunga Zambia kwa mikwaju ya penalti 4-3 katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Nelson Mandela Bay baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya goli 1-1.

Katika mchezo huo, Zambia walikuwa wa kwanza kupata goli lililofungwa dakika ya 19 na mshambuliaji Comfort Seleman ambaye alitumia vizuri makosa ya safu ya ulinzi ya Tanzania baada ya kuondoka na mpira kuanzia katikati ya uwanja hadi kwenye goli na kupiga shuti  ambalo lilimsinda golikipa Aisha Mrisho.

Lakini kipindi cha pili Tanzania ilisawazisha bao hilo kwa mkwaju wa penalti iliyopigwa na Koku Kipanga baada ya Aisha Masaka kuchezewa madhambi ndani ya eneo la 18 na mchezo huo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.

Akizungumza mara baada ya kuipokea timu hiyo, Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Wallece Karia amesema kuwa, wakati timu hiyo inaondoka aliwataka wachezaji hao pamoja na wale wa timu ya wakubwa, Twiga Stars kuhakikisha mmoja wao wanarudi na kombe hilo ikiwa kama zawadi kwa viongozi wapya wa serikali waliopata ushindi wa kishindo.

Amesema, anafurahi kwa kuwa timu hiyo imekuwa ya kwanza kutoa zawadi ya ushindi kwa viongozi hao na jambo kubwa kwa sasa ni kuomba kupata sapoti kwaa ajili ya vijana hao wa kike na kiume kwani ndio msingi wa timu nzuri za Taifa kwa miaka ijayo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Hukumu ya Bernard Morrison kutolewa leo

Kesi inayomuhusisha aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Yanga ambaye kwa hivi sasa anakipiga Simba Sc, Bernard Morrison itasikilizwa na

Read More...

Kamanda wa AFRICOM azuru Tanzania akiangazia ushirikiano katika nyanja ya usalama

Kamanda wa Kamandi ya Afrika ya Jeshi la Marekani (AFRICOM) Jenerali Stephen Townsend, alikuwa na ziara ya siku

Read More...

TETESI ZA SOKA ULAYA

Paris St-Germain imeanza mazugumzo ya awali na Paul Pogba kuangalia kama anaweza kujiunga nao kutoka Manchester United msimu huu

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu