Trump aalikwa kuhudhuria kikao cha tuhuma zinazomkabili.

In Kimataifa, Siasa

Bunge la Congress nchini Marekani limemualika rais wa nchi hiyo Donald Trump katika kikao chake kitakachosikiliza tuhumazinazomkabili rais huyo tarehe 4 Disemba.

Jerrold Nadler, mwenyekiti wa chama kamati ya Congress ya masula ya sheria kutoka chama cha Democratic, alisema kuwa Bwana Trump anaweza kuhudhuria au ”akome kulalamika juu ya mchakato” huo.

Kama atahudhuria, rais ataweza kuwahoji mashahidi.

Kikao hicho kitakua ni hatua itakayowezesha kuanzishwa kwa hatua nyingine katika mashtaka , yanayomuhusisha na Ukraine chanzo chake ni simu ambayo rais Trump alimpigia rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky.

Katika mawasiliano ya simu hiyo Trump alimtaka Bwana Zelensky amchunguze Joe Biden, ambaye kwa sasa ndie mgombea aliye mstari wa mbele kuwania kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Democratic katika uchaguzi wa urais mwaka ujao, na mtoto wake wa kiume Hunter Biden, ambaye awali alifanyia kazi kampuni ya nishati ya Ukraine Burisma.

Uchunguzi unataka kubaini juu ya ikiwa Bwana Trump alitumia tisho la kuzuwia msaada wa jeshi la Marekani kwa Ukraine ili kuifanya imchunguze Biden na mwanae. Rais Trump amekana kufanya kosa lolote na ameutaja uchunguzi kuwa ni ” hila”.

Wiki iliyopita, Kamati ya masuala ya ujasusi ilikamilisha wikimbili za kusikiliza , kufuatia wiki kadhaa za vikao vya faragha ambapo waliwahoji mashahidi.

Adam Schiff, mwenyekiti wa kamati ya ujasusi, anayeongoza uchunguzi huo alisema kamati za masuala ya kigeni na intelijensia – sasa zinaifanyia kazi ripoti yao, ambayo itatolewa tarehe 3 Disemba.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu