Trump apewa onyo

In Kimataifa

Rais mteule wa Marekani, Joe Biden ameonya kuwa hatua ya Rais Donald Trump kukataa kukubali kushindwa na kuratibu mchakato wa kipindi cha mpito cha kukabidhi madaraka, inaweza kusababisha watu zaidi kufa kwa ugonjwa wa COVID-19. Akizungumza na waandishi habari kwenye jimbo la Delaware, Biden amesema watu wengi huenda wakafa iwapo hakutakuwa na ushirikiano. Serikali ya Trump bado haijamkubali rasmi Biden kama rais mteule, hatua inayomaanisha kuwa Biden na timu yake hawawezi kupata taarifa za kijasusi kuhusu masuala ya usalama wa taifa, vile vile kuwa na mpango wa kusambaza chanjo zinazowezekana za COVID-19. Biden amesema wanapopambana na COVID, wanapaswa kuhakikisha kwamba wafanyabiasha na wafanyakazi wana rasilimali na mwongozo wa kitaifa. Biden na Makamu wa Rais mteule, Kamala Harris pia walifanya mikutano kwa njia ya video na vyama vya wafanyakazi na wakuu wa kampuni mbalimbali.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Dk. Bashiru Awakaribisha CCM Wanawake Imara wa Upinzani.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashiru Ali, amesema chama chake kinawakaribisha wanasiasa wanawake ‘shoka’ wa upinzani

Read More...

TRUMP KUNG’ATUKA RASMI IKULU

Rais wa Marekani Donald Trump amesema jana kwamba ataondoka ikulu ya White House baada ya rais mteule Joe

Read More...

SOKA NA TETESI ZAKE ULAYA

Pep Guardiola anataka Manchester City kumsajili Jack Grealish, baada ya kubaini kiungo huyo wa kati wa Aston Villa na

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu