TRUMP KUNG’ATUKA RASMI IKULU

In Kimataifa

Rais wa Marekani Donald Trump amesema jana kwamba ataondoka ikulu ya White House baada ya rais mteule Joe Biden kuthibitishwa rasmi mshindi wa uchaguzi, na kurudia kwamba hatakiri kuwa ameshindwa uchaguzi huo.Alipoulizwa na waandishi wa habari kama ataondoka White House iwapo kamati ya wajumbe maalumu maarufu Electoral College itathibitisha ushindi wa Biden, Trump alikiri kuwa ataondoka, ingawa alisema iwapo wajumbe hao watamthibitisha watakuwa wamefanya kosa na kuongeza kuwa itakuwa vigumu kukubali. Amerudia madai yake kwamba kulikuwa na udanganyifu kwenye uchaguzi huo, ingawa kwa mara nyingine hakuweza kuthibitisha madai yake. Kwenye mkutano na waandishi wa habari katika kuadhimisha sherehe za Siku ya Shukrani, Trump alifikia hatua ya kuifananisha miundombinu ya uchaguzi wa Marekani na ya mataifa ya ulimwengu wa tatu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

RAIS MAGUFULI AZINDUA SHAMBA LA MITI SILAYO

Rais Dk John Magufuli leo amezindua na kubadilisha jina Shamba la Miti Chato na kuliita Shamba la Miti

Read More...

Kenya kutumia Teknolojia ya Roboti kudhibiti Corona.

Wizara ya Afya nchini Kenya imezindua Teknolojia ya kutumia Roboti ili kupambana na janga la virusi vya Corona na

Read More...

Rais wa Ethiopia atua Chato kwa ziara ya siku moja.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la watu wa Ethiopia Sahle Work Zewde,amewasili nchini Tanzania tayari kufanya ziara

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu