TRUMP KUTIMULIWA TENA.

In Kimataifa

Wademocrat nchini Marekani wamesema wanaendelea na shinikizo lao la kutaka kumuondoa Rais Donald Trump madarakani katika siku zake za mwisho za utawala wake, baada ya wafuasi wake kuvamia majengo ya bunge wiki iliyopita, huku warepublican wengine pia wakiunga mkono juhudi hizo.Spika wa bunge Nancy Pelosi amesema kutakuwa na azimio leo la kulitaka baraza la mawaziri kumuondoa Trump ofisini kutumia kipengee cha 25 cha katiba kwa msingi wa kutoweza kutekeleza majukumu yake. Pelosi amesema ikiwa Makamu wa Rais Mike Pence hatatumia kipengee hicho, basi watawasilisha hoja bungeni ya kushinikiza atimuliwe. Seneta wa chama cha Democratic Chuck Schumer ameonya kwamba bado kuna kitisho kikubwa cha vurugu kutoka kwa makundi yenye misimamo mikali, kufuatia tukio la wiki jana mjini Washington. Schumer amesema wiki chache zijazo ni muhimu katika mchakato wa demokrasia nchini Marekani ambapo rais mteule Joe Biden na makamu wake Kamala Harris wataapishwa kama rais na makamu Januari 20. Wakati huo huo, seneta mwengine tena wa chama cha Republic pia amemtaka Rais Donald Trump ajiuzulu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

RAIS MAGUFULI AZINDUA SHAMBA LA MITI SILAYO

Rais Dk John Magufuli leo amezindua na kubadilisha jina Shamba la Miti Chato na kuliita Shamba la Miti

Read More...

Kenya kutumia Teknolojia ya Roboti kudhibiti Corona.

Wizara ya Afya nchini Kenya imezindua Teknolojia ya kutumia Roboti ili kupambana na janga la virusi vya Corona na

Read More...

Rais wa Ethiopia atua Chato kwa ziara ya siku moja.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la watu wa Ethiopia Sahle Work Zewde,amewasili nchini Tanzania tayari kufanya ziara

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu