Trump kuzungumza na Iran

In Kimataifa

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa yuko tayari kufanya mzungumzo na viongozi wa Iran, kama watamtafuta. Akizungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ya Marekani, Trump alisema anatarajia viongozi wa Iran wampigie simu. Aidha rais huyo amesema kuwa aliamuru kupelekwa kundi la manowari zinazobeba ndege za kivita katika Ghuba ya Mashariki ya Kati kwa sababu ya vitisho vya Iran. Mwaka jana, Trump alijiondoa kutoka mkataba wa nyuklia na Iran na kisha akaongeza vikwazo dhidi ya nchi hiyo. Umoja wa Ulaya umetoa wito wa kuwepo suluhisho la kidiplomasia kwa mzozo huo. Hapo jana, viongozi wa jumuiya hiyo wakiongozwa na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel walisisitiza kuhusu dhamira yao ya kuuheshimu muafaka huo wa mwaka wa 2015, lakini wakasisitiza kuwa hawatakubali masharti yoyote.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

SOKA LA KIMATAIFA NA FUNUNU ZAKE

Real Madrid bado wanataka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Brazili Neymar, lakini wanataka hakikisho kutoka Paris St-Germain kuhusu hali

Read More...

(TAMISEMI) KUTOA TANGAZO LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani S Jafo kesho tarehe 23 Mwezi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu