Tuko imara hatuyumbishwi – Afunguka Mchungaji Peter Msigwa.

In Kitaifa, Siasa

Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia tiketi ya CHADEMA, Mchungaji Peter Msigwa amewaaminisha wafuasi wa chama hicho mkoani humo kuwa kipo imara na wala hakiteteleki na ongezeko la wimbi la madiwani na wabunge wao wanaohamia Chama cha Mapinduzi.

Mhe. Peter Msigwa

Msigwa amesema iko haja ya wananchi kuwapuuza viongozi hao wanaohama vyama kwani wameshindwa kuwa na utu na kuheshimu heshima kubwa waliyopewa na Watanzania kuwaongoza na badala yake wanakimbia majukumu.

Hao watu ni wa kupuuzwa na wala hii si habari mpya kwetu tunajua nini wanafanya lakini niwaambie wana Iringa mimi na chama changu tuko imara hatuyumbishwi na hao wachache wanaoondoka na tutaendelea kuwatumikia kwa moyo mmoja,” amesema Mchungaji Msigwa kwenye mahojiano yake na gazeti la Mtanzania.

Mhe. Msigwa amesema hayo ikiwa ni siku moja tu imepita baada ya Diwani wa Kata ya Gangilonga ambaye pia alikuwa ni Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Dady Igogo kutangaza kujiuzulu nafasi hiyo ya udiwani na kuwa raia wa kawaida.

Katika hali ya kushangaza Igogo ameeleza kuwa sababu za kujiuzulu kwake ni kutokana na kupitia kipindi kigumu kwenye siasa pia ni faida kwa usalama wa maisha yake.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu