TUME YA MADINI YAZIDI KUIPAISHA SEKTA YA MADINI

In Uchumi

Mnada wa kwanza wa almasi tangu kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika wafanyika..
Wafanyabiashara wa madini wapongeza Wizara ya Madini, Tume ya Madini

Tume ya Madini kupitia Ofisi ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Shinyanga leo tarehe 18 Februari 2019 imeweka historia ya nchi baada ya kufanya mnada wa asilimia tano ya madini ya Almasi kutoka Mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo mkoani Shinyanga.

Akizungumza kupitia mahojiano maalum, Meneja wa Biashara ya Madini wa Tume ya Madini, George Kaseza amesema kuwa uuzaji wa asilimia tano ya almasi kutoka mgodi wa WDL ni matokeo ya maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Madini, Doto Biteko kupitia mkutano wake alioufanya mwaka jana na wadau wa madini mkoani Shinyanga.

Ameeleza kuwa, kupitia mkutano husika ilikubalika mgodi wa WDL kuuza asilimia tano ya almasi yake kwa wafanyabiashara wadogo wa madini ili waweze kwenda kuuza kwenye Soko la Kimataifa la Dhahabu na Almasi la Shinyanga na kujipatia kipato huku wakilipa kodi mbalimbali Serikalini.

Amesema mgodi wa WDL ulianza kwa kujenga kituo ndani ya eneo lake ambapo kwa kuanzia mnada umeanza kufanyikia hapo.

Kaseza amewataka wafanyabiashara wadogo wa madini ya almasi na dhahabu nchini kuyatumia masoko yaliyoanzishwa hivi karibuni.

Wakizungumza katika nyakati tofauti wafanyabiashara wadogo wa madini ya almasi wamepongeza Serikali kupitia Wizara ya Madini na Tume ya Madini na kuongeza kuwa mbali na kujipatia kipato wataanza kulipa kodi mbalimbali Serikalini.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WAGONJWA WA CORONA WAFIKIA 13 TANZANIA

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema idadi ya wagonjwa wa corona imefikia 13 ambapo kati yao 8 ni

Read More...

CORONA HAITAZUIA KUFANJIKA KWA UCHAGUZI – JPM

Rais Dkt. John Pombe Magufuli, amesema Ugonjwa wa Corona hautaizuia Tanzania kufanya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu. Rais

Read More...

Mshtakiwa wa mauaji ya mfanyakazi wake wa Ndani, apandishwa kizimbani

Mshtakiwa wa mauaji ya mfanyakazi wake wa Ndani Mkami Shirima(30)Mkazi wa Sakina Arusha amefikishwa tena katika mahakama ya hakimu

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu