Matokeo ya awali, ambayo yalipangwa kutolewa leo Jumapili, sasa yatatolewa wiki ijayo, mkuu wa tume ya uchaguzi nchini humo CENI ameliambia shirika la habari la AFP masaa machache kabla ya muda wa mwisho kumalizika.
“Haitawezekana kutangaza matokeo siku ya Jumapili. Tunapinga hatua , lakini hatuna kila kitu bado,” alisema Corneille Nangaa, bila ya kutangaza siku ya kutangaza matokeo hayo.
Kanisa katoliki lenye ushawishi nchini Congo, ambalo limetoa zaidi ya wachunguzi wa uchaguzi 40,000 , lilisema siku ya Alhamis kwamba linamjua mshindi wa uchaguzi huo , lakini halikumtaja.