Tunisia yazidi kuzama katika mgogoro

In Kimataifa

Rais wa Tunisia Kais Saeid amemtimua waziri wa ulinzi siku moja tu baada ya kumfukuza waziri wake mkuu Hichem Mechichi na kulisimamisha bunge kwa mwezi mmoja na hivyo kuitumbukiza nchi yake katika mgogoro wa kikatiba. Waziri mkuu aliyetimuliwa Hichem Mechichi amesema atakabidhi mamlaka kwa mtu atakayeteuliwa. Wakati huo huo waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amemtaka rais wa Tunisia aheshimu demokrasia na awe tayari kwa mdahalo na pande zote. Umoja wa Ulaya pia umetoa wito kwa watu wa Tunisia juu ya kuheshimu utawala wa kisheria na kuepusha umwagaji damu. Uamuzi uliowashangaza wengi wa Rais Saied unafanyika katika kipindi cha takribani muongo mmoja tangu mapinduzi ya Tunisia ya 2011, ambayo yalikuwa chachu ya vuguvugu la mataifa ya Kiarabu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Tetesi za Soka Ulaya leo Alhamisi Septemba 23, 2021

Mshambuliaji wa Arsenal na Ufaransa Alexandre Lacazette, 30, hana hamu ya kusaini kandarasi mpya klabuni hapo. Mkataba wake wa

Read More...

Wanaharakati wa haki za binadamu wahoji hukumu dhidi ya Rusesabagina

 Makundi ya kutetea haki za binadamu barani Afrika yamelalamikia uamuzi wa mahakama kuu ya Rwanda ya kumfunga jela kwa miaka 25, Paul Rusesabagina ambaye alisifika sana kwenye filamu ya Hollywood ya Hotel Rwanda.  Mahakama hiyo Jumatatu ilisema kwamba imepata Rusesabagina pamoja na washukiwa wengine 20 na hatia ya

Read More...

LISSU NA WENZAKE WAFUTIWA KESI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeifutia kesi ya uchochezi iliyokuwa inamkabili Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleao

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu