Uchaguzi DRC: Kura yaahirishwa mpaka mwezi machi kwa majimbo matatu, wagombea saba wa upinzani walia na tume.

In Kimataifa

Mustakabali wa uchaguzi nchini Jamuhuri ya Demokrasi ya Congo (DRC) wazidi kuingia dosari baada ya tume ya uchaguzi leo Disemba 26 kutangaza kuahirishwa upigwaji kura katika mikoa mitatu mpaka mwezi machi 2019.

Kura hiyo ambayo ilitakiwa kupigwa Disemba 23 mwaka huu iliahirishwa kwa wiki moja mpaka Disemba 30, yaani Jumapili ijayo. Hata hivyo uchaguzi huo tayari umeshacheleweshwa kwa miaka miwili sasa, huku wapinzani na wanaharakati wakimlaumu rais amalizaye muda wake Joseph Kabila kwa kutafuta visingizio kusalia madarakani. Mgombea wa chama tawala Ramazani Shadary ni mshirika mkubwa wa Kabila na inatarajiwa ataendelea kulinda maslahi ya Kabila akiingia madarakani.

Maeneo hayo matatu ambayo yanaonekana kuwa ni ngome za upinzani ni Beni na Butembo kwa upande wa mashariki ambayo yamekuwa yakipambana na milipuko ya ugonjwa hatari wa Ebol toka mwezi Agosti mwaka huu.

Eneo la tatu ni Yumbi lilopo magharibi mwa nchi ambapo watu zaidi ya 100 wameuawa wiki iliyopita katika makabiliano ya kikabila.

Shughuli za uchaguzi katika sehemu nyengine zote zilizobaki za nchi hiyo kubwa zitaendelea kama ilivyopangwa siku ya jumapili.

Matokeo ya uchaguzi wa maeneo hayo matatu hayataathiri mbio za urais kwa sababu mshindi atatangazwa Januari 15 na kuapishwa Januari 18.

Katika taarifa yake, tume ya uchaguzi (CENI) imesema hatua hiyo inatokana na kusambaa kwa Ebola katika maeneo ya Beni na Butembo pamoja na kudorora kwa amani katika maeneo hayo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

TCRA yatoa leseni 224 za watoa huduma za maudhui mtandaoni…93 ni za Blogs, 97 ni za Online Tv.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba amesema leseni 224 zimetolewa kwa watoa huduma

Read More...

Muungano wa Afrika umeiomba DR Congo uahirishe kutangaza matokeo kamili ya uchaguzi mkuu

Muungano wa Afrika (AU) umeitaka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo iahirishe kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu. Muungano huo unaonuia

Read More...

Bunge kupiga kura tena 29 mwezi januari.

Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ataitisha kura nyingine Januari 29 kuhusu makubaliano ya Uingereza kujitoa kutoka Umoja wa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu