Uchumi wa Zanzibar waimarika, Shein atangaza Elimu bure.

In Kitaifa, Uchumi

Sherehe za miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar zimefanyika leo Januari 12, 2018 katika Uwanja wa Amani, Visiwani Zanzibar, ambapo viongozi wakuu wa nchi wamehudhuria pamoja na mamia ya wananchi.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria ni Mgeni Rasmi ambaye ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Bi. Samia Suluhu, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Seif Ali Iddi, Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na wengine.

Akihutubia katika Sherehe hizo, Dkt. Shein amesema:

“Serikali zote saba ambazo zimehudumu baada ya mapinduzi zimefanya mengi ya kuwaletea maendeleo Wazanzibari. Katika mwaka 2017, mapato yameongezeka kwa shilingi bilioni 61.097 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2016 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 12.5.

“Kasi ya ukuaji wa uchumi wetu imeongezeka kwa asilimia saba kwa mwaka 2017 ikilinganishwa na asilimia 6.8 mwaka 2016, pato la mtu binafsi limeongezeka kufikia Sh. 1,806,000 ikilinganishwa na Sh. 1,632,000. Idadi ya watalii visiwani Zanzibar imeongezeka kwa asilimia 14.2 kutoka watalii 379,242 mwaka 2016 hadi kufikia watalii 433,116 mwaka 2017.”

Dkt. Shein aliyeongoza sherehe hizo ikiwemo kukagua gwaride maalumu lililoandaliwa katika sherehe ametangaza rasmi serikali yake itaanza tena kutoa elimu ya sekondari bure kuanzia mwezi Julai mwaka huu huku akiwataka wananchi kuunga mkono juhudi za serikali za kuwaletea maendelo thabiti wananchi wake.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Msako mkali dhidi ya makanisa ya kikristo umeanza China na kuzua taharuki

Hatua ya hivi karibuni ya msako mkali unaotekelezwa na polisi dhidi ya makanisa nchini China umesababisha taharuki kubwa kwamba

Read More...

Mshauri wa zamani wa usalama wa Trump kuhukumiwa.

Mshauri wa zamani wa usalama wa taifa nchini Marekani Michael Flynn anatarajiwa kuhukumiwa leo katika mahakama kuu mjini Washington

Read More...

Jose Mourinho atimuliwa Manchester United.

Jose Mourinho amefutwa kazi wadhifa wake kama meneja wa Manchester United. Klabu hiyo imetangaza kwamba ameondoka katika klabu hiyo

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu